Sammy Kibet (22) kutoka Elgeyo Marakwet alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mkewe Mercy Kiplangat (21) ambaye alimuacha takriban wiki mbili zilizopita.
Kibet alisema ndoa yake ya chini ya mwaka mmoja ilivurugika mwezi uliopita baada ya mkewe kugundua ana mpango wa kando. Alisema mkewe alitoroka kurudi kwao akiwa na ujauzito wa mwezi mmoja.
"Nilikuwa nimeenda Eldoret kidogo kwa ajili kazi. Wakatu nikiwa kwa nyumba, bibi yangu alianza kushuku niko na mpango wa kando. Kweli alinipata na mwanamke mwingine kisha akaenda kwao nyumbani. Sasa hivi ako kwao," Kibet alisema.
Alifichua kwamba alikuwa amemuajiri mwanamke ambaye alikuwa na mahusiano naye.
"Mwenye ambaye nilipatikana na yeye alienda kwao Meru. Alikuja kuniomba kazi akisema hana kazi. Bibi yangu alimfukuza huyo wa Meru akaenda kwao. Alikuwa awe mfanyikazi wetu, bibi akanipatana na yeye," alisema,
Alisema juhudi za kurejesha mahusiano yake na mkewe hazijaweza kufua dafu na kudai kuwa Mercy tayari amemblock.
.
"Huwezi kunipatanisha mimi kwa Radio Jambo. Ungenipigia simu. Hata vile unaongea huko serious. Pigia huyo mwanamke ako Meru muendelee. Siwezi kurudi saa hii. Ukuje kwetu ndio tujue uko serious," Mercy alisema.
Mercy aliendelea kumshutumu mumewe kwa kudanganya kuhusu maelezo kadhaa ambayo alitoa hewani.
"Ako na mpango wa kando. Nikitaka kumrudia, ako na msichana kutoka Meru. Akipigiwa simu anatoka nje. Huyu msichana anashinda naye. Nikikuja nyumbani, mimi ndiye naingia, huyo anatoka. Amove on, hivyo tu. Vile anaongea hayuko serious. Kuhusu mimba, tutang'angana. Anipigie simu," Mercy alisema.
Kibet alimwambia, "Nataka nikuombe msamaha. Mimi niko serious. Naomba arudi tukae maisha mazuri. Mimi bado nakupenda, wewe ni mke wangu. Hakuna mtu mwingine. Nakupenda sana kama mke wangu. Naomba urudi nyumbani tuendelee na maisha,"
Mercy ambaye alizungumza kwa ukali alimwambia mumewe, "Najua unalia, ongeza sauti na utume transport saa hii nikuje hapo saa hii. Uko kazi unatuma transport!!"
Gidi aliwaagiza wawili hao kuzungumza zaidi baada ya Patanisho na kupanga jinsi ya kurudiana.
Hata hivyo alishangazwa sana na ukali wa Mercy na kusema, "Nani ndiye bwana hapa?,, Mara anasema utume transport na umesema humtaki. Huyu Kibet aende tu Meru. Vile Mercy anaongea, he is a very tough woman na hapendi jokes!"
Ghost alisikika kukubaliana naye, "Mercy ndiye bwana hapa!"