logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Hajapeleka hata paka, mbwa kwetu!" Mke amkana mumewe anayetaka kurudi baada ya kumtenga miaka 30

Bi Grace alisema bado hajafikiria ikiwa atakubali ombi la msamaha la mumewe.

image
na Samuel Maina

Vipindi06 November 2023 - 06:35

Muhtasari


  • •Bw Samuel alisema ndoa yake ya miaka 30 ilianza kuyumba baada ya mwanawe kuhamia jijini Nairobi ambapo mkewe alianza kumtenga.
  • •Bi Grace alikiri kwamba makosa ya Bw Samuel ni mengi na kuweka wazi kuwa hamtambui kama mumewe.
GHOST NA GIDI STUDIONI

Bw Samuel Omukaya ,50, kutoka Busia alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Grace Ahonyo Osome ,45, ambaye alikosana naye zaidi ya miaka sita iliyopita.

Bw Samuel alisema ndoa yake ya miaka 30 ilianza kuyumba baada ya mwanawe kuhamia jijini Nairobi ambapo mkewe alianza kumtenga.

"Mimi naishi Nairobi, mke wangu alikuwa anaishi nyumbani. Hapo awali alikuwa ananitembelea, wakati kijana alikataaa shule, nilimwambia amlete nimtafutie course. Nilimpeleka mtoto kozi ya welding akapata kazi na nyumba. Baadaye mke wangu akawa hanitembelei tena anatembelea mtoto. Mahitaji yake yote ameweka kwa mtoto wetu. Sasa ni zaidi ya miaka zaidi ya sita tangu tukosane," Bw Samuel alisimulia.

Aliongeza, "Nilipigiwa simu nikaambiwa anataka kuuza shamba. Nyumba ya kwanza ilianguka kijana akamjengea nyingine.Wakati wa matanga ya dadangu nilienda nyumbani akafunga mlango nisiingie kwa sababu sio mimi nilijenga. Lazima nyumba ifanyiwe mila ndo niingie, saa hii siwezi kuingia... Hivi majuzi alituma mtoto ambaye napenda zaidi akamwambia akuje anidanganye ati anaenda Pwani nimpatie kitambulisho. Nilimwambia kitambulisho changu kilipotea akasema atanipeleka Huduma Centre tuandikishe kingine.  Mtoto alinikumbatia, akanichekesha mpaka nikaenda Huduma Centre naye tukaandikisha kitambulisho. Hata hakungoja kitambulisho kitoke, alienda na waiting card. Kumbe kitambulisho ilikuwa inahitajika ndio auze shamba. Mtoto alisema walikuwa wanataka kuuza shamba alipiwe masomo."

Samuel pia aliibua madai kuwa kuna shemeji yake ambaye alichangia katika mzozo wake na mkewe na kuwatenganisha.

"Kuna ndugu mmoja tumeoa mahali moja na yeye. Nilikuta ni yeye alikuwa anamharibu. Alikuwa anasema nitafute bibi mwingine nimjengee nyumba nyingine. Nilikataa kwa sababu shamba ni ndogo. Siku ingine akaniomba namba ya simu ya mke wangu. Akawa anamuuliza bibi maswali alafu ananipatia niongee na yeye," alilalamika.

Bi Grace alipopigiwa simu mwanzoni alimkana mumewe na kukata simu mara moja.

Baadaye alipokubali kushika simu alikiri kwamba makosa ya Bw Samuel ni mengi na kuweka wazi kuwa hamtambui kama mumewe.

"Hakuna chenye nasema. Simtambui kama mume wangu. Makosa yake ni mengi. Hajawahi kushughulika. Watoto ni wakubwa sihitaji msaada wa mtu. Hakuna kijana ananisaidia najisaidia mwenyewe. Nyumba najijengea mwenyewe," Grace alisema.

Aliongeza, "Ni mtu ambaye hajapeleka hata pussy pekee yake nyumbani kwetu, alafu ajiite bwana?? Hata mbwa pekee yake hajawahi kupeleka. Hiyo ilikuwa urafiki na iliisha. Hakuna usaidizi, hiyo miaka yake alikuwa anaishi Nairobi na wanawake, anaoa hadi wale wako na watoto. Hajawahi kusaidia watoto."

Bw Samuel alijitetea kwa kusema, "Ile hasira nilikuwa nayo nimekuta ni watu walikuwa wanataka kunikosanisha naye. Nimemsamehe naomba anisamehe. Nairobi ililkuwa ni hali tu ya kutafuta."

Bi Grace alisema bado hajafikiria ikiwa atakubali ombi la msamaha la mumewe.

"Amekuwa akitafutia nani? Saa hii maisha imemlea anataka arudi nimlishe, siwezi!" Grace alisema.

Ujumbe wa kumalizia, Samuel alisema, "Najua vizuri yeye ni mke wangu, mama ya watoto wangu. Sina mwingine ambaye niko naye."

Grace alisema, "Hakuna jambo nitamwambia. Anisahau kabisa."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved