Jumatano asubuhi, jamaa aliyejitambulisha kama Victor Juma ,33, kutoka Nairobi alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Eunice Nanjala ,27, ambaye alikosana naye mwezi uliopita kuhusiana na mambo ya mpango wa kando.
Victor alisema ndoa yake ya miaka mitano ilivunjika baada ya mkewe kupata jumbe zake na mpango wa kando kisha akatoroka.
Katika utetezi wake, alidai hakuwa na mpango wa kwenda nje ya ndoa ila alipata vishawishi vya mtandaoni kuhusu kuchumbiana na Mkamba.
"Mimi sikuwa mtu wa kuingia hapo lakini ni vile nilipata mambo ya Facebook. Nilisoma mahali mitandaoni ati kama hujawahi date Mkamba hujawahi kudate. Mpango wa kando ilikuwa mambo na Mkamba. Nilipoona posti hiyo na nikaona watu wengi wanachangia, niliamua kujaribu pia," Victor alisimulia.
Aliongeza, "Sasa ni ile kuna mama wa ploti alikuwa anaitwa Mwende nikajaribu naye alafu ndio nikashikwa. Alipopata hizo jumbe za simu alitoroka. Sasa hivi yuko Nakuru. Nikimpigia ananiambia nibaki na mipango wa kando."
Aliweka wazi kwamba ana watoto wawili na Bi. Eunice, wote ambao aliwabeba.
Eunice alipopigiwa simu alimshtumu mumewe kwa ujeuri na akabainisha wazi kuwa ame'cheat mara kadhaa katika ndoa yao.
"Mtu akianza ukora ama akianza kujifanya kuwa na Mwerevu unamuacha tu na hiyo werevu yake. Niliona ajipange na hao mipango wa kando alafu wakati ataamua kutulia atatutafuta," Eunice alisema.
Aliongeza, "Huyo anajifanya jogoo wa mjini. Mpango wa kando si mmoja tu, ni kadhaa. Mpaka unapata anakuja nyumbani na viatu za rubber za wanawake za ngoma na hakuwa ametoka nazo. Anakuja amejipaka marashi ya wanawake na akitoka hakuwa amejipaka na pia hakuna pesa nyumbani. Nikimuuliza alinunua marashi kwa nini na nyumbani hakuna chakula nasema ati marashi alipakwa kwa gari."
Bwana Victor hata hivyo alisisitiza kwamba alikuwa na mpango wa kando mmoja tu.
"Rudi kwa huyo Mama Njunge mkajipake marashi na yeye kwa sababu uliona huna haja ya familia," Bi Eunice alimwambia.
"Nilipata message unasifu huyo mwanamke vile amekupikia nyama na mimi nakupikia chai na mrenda. Wanaandikia message ati vile alimpikia vizuri."
Victor alijitetea kwa kusema, "Marashi ata niko nayo kazini, ile kidogo kidogo nikisweat najipaka. Naomba urudi sitarudia. Eunice kweli nilikosa, nimekubali makosa yangu. Niligundua wewe ndo mzuri kuliko hao wanawake."
Eunice alisema, "Alete ng'ombe nyumbani. Akishafanya hivyo, maneno mengine baadaye."