logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa akataa kumsaidia mtoto wa mkewe baada ya kudaiwa alitoa mimba

Saul alifunguka kuhusu tatizo lingine katika mahusiano yao akieleza kuwa Bi Purity alikuwa amekataa kuzaa naye.

image
na Samuel Maina

Vipindi09 January 2024 - 06:13

Muhtasari


  • •Saul alisema mahusiano yao ya takriban miaka mitano yalisambaratika mwaka wa 2020 baada ya mkewe kuenda Uarabuni, kinyume na matakwa yake.
  • •"Ajirekebishe kwanza. Sioni haja ya mahusiano ambapo uko na mtoto alafu mtu wako hataki mtoto wako," Purity alisema.

Jamaa aliyejitambulisha kama Saul Ambaso Makwacha ,28, kutoka Kakamega alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mchumba wake Purity Kerubo ,26, ambaye alikosana naye takriban miaka mitatu iliyopita.

Saul alisema mahusiano yao ya takriban miaka mitano yalisambaratika mwaka wa 2020 baada ya mkewe kuenda Uarabuni, kinyume na matakwa yake.

"Kuna hii mpango ya kuenda Saudia. Wakati alianza kupanga kuenda, nilikuwa nimemkanya nikamwambia nitashughulikia kila kitu kwa nyumba. Hata hivyo alienda. Kwa sasa yuko kwao alirudi," Saul alisimulia.

Aliongeza, "Tumekuwa tukizungumza. Lakini haongei ukweli. Aliniambia niende kwao tukutane. Nikajipanga, ilikuwa tarehe 25 akaniambia kuna mkutano wa ukoo. Akasema tukutane tarehe moja. Tarehe moja alikuwa amezima simu, yuko mteja na ameniblacklist. Kulinga na jinsi tunavyoongea, kuna matumaini."

Saul pia alifunguka kuhusu tatizo lingine katika mahusiano yao akieleza kuwa Bi Purity alikuwa amekataa kuzaa naye.

"Kuna mtoto wake ambaye nilikuwa nimemuoa na yeye. Tulikuwa tunasumbuana na yeye upande wa mtoto. Hatukuwa na mtoto pamoja. Kuna vile nilimtetesha. Alitaka nimsaidie mtoto wake . Nilimwambia anizalie mtoto ndio nishughulikie huyo wake, alikataa akasema nishughulikie huyo wake kwanza. Nilikuwa nampenda huyo msichana. Hata nikipata mwingine, bado namuwaza, sijui shida ni nini," alisema.

Purity alipopigiwa simu alisema, "Ajirekebishe kwanza. Sioni haja ya mahusiano ambapo uko na mtoto alafu mtu wako hataki mtoto wako. Ni heri nikuwe na mtoto kuliko mtu ambaye ananitaka lakini hataki mtoto."

Saul alisema, "Tumekaa karibu miaka tatu. Mimba ya kwanza alitoa. Kulingana na marafiki, waliniambia bibi yangu alitoa mimba. Nilikuwa nishaanza kumpeleka clinic. Nilikuwa nashughulikia mtoto, akaenda kwao. Kila mara tukikosana, akipigia mama yake, mara moja alikuwa anamtumia nauli. Sababu niliacha kumsaidia mtoto wake ilikuwa hiyo kutoa mimba. Nikasema siwezi kumsaidia."

"Pia Ilisemekana anaongea na baba mtoto. Nikamwambia nitamsaidia kila kitu kwa nyumba. Lakini mambo ya mtoto, sitamkataza kuongea na baba mtoto. Baada ya hapo nikaacha kushughulikia mtoto. Akampeleka nyumbani kwao."

Je, ushauri wako kwa wawili hao ni upi?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved