Mwanadada ambaye lajitambulisja kama Zainab Nakami ,23, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake John Muyekho ,33, ambaye alikosana naye mwezi Mei mwaka uliopita.
Zainab alisema aligura ndoa yake ya mwaka mmoja akiwa mjamzito kufuatia tabia ya mumewe kuchelewa nje usiku na wakati mwingine hata kutorudi nyumbani.
Aidha, alidai kwamba wakati akiwa mjamzito alishindwa kuishi na John kwani alihisi mwili wake ukimpinga.
"Nilikuwa nimeolewa. Ilikuwa 2022 mwezi wa nane. Akanipatia ball ya kwanza ikatoka. Nilienda kwetu alafu nikarudi huko 2023 mwezi wa pili. Mwezi wa tatu nikapata ball ingine. Mwezi wa sita, kawa kwa nyumba hatuelewani, ikawa kwa nyumba ananitusi.
Mimba yangu pia ikamkataa nikaamua niende kwetu. Nilihis simtaki, alikuwa ananiudhi. Kufuatia hayo nilifunga virago vyangu nikaenda nyumbani. Nikimpigia simu kumuitisha pesa ya clinic anasema ati mimi mwenyewe ndiye nilitoka," Zainab alisimulia.
Aliongeza, "Wakati nikujifungua, Walikuja na mama yake hospitali kuniona lakini hawakuja na chochote. Baada ya kujifungua, nikimuitisha pesa ama nimwambie mtoto ni mgonjwa anasema hana pesa. Aliona tu mtoto lakini kumshika hapana.Nilimpigia simu nikamwambia nataka kurudi kwa ndoa alisema mimi mwenyewe ndiye nilitoka Wakati fulani alinitumia ujumbe akaniambia mimi bado ni mkewe nisiwe na wasiwasi..Wazazi wake wanataka nirudi nyumba lakini yeye haeleweki. Si mkora lakini anasumbua sumbua. Kuna wakati alisema nipeleke mtoto akanyolewe lakini yeye hakuwepo. Mama alinyoa mtoto bila John kuwa nyumbani."
Kwa bahati mbaya, Zainab hakuweza kupatanishwa na John kwani juhudi za Gidi kumtafuta mzazi huyo mwenzake hazikufua dafu.
Zainab alisema, "Mimi nimejiharibia maisha na yeye ndiye alifanya. Huko kwetu ni mimi pekee ndiye sijaenda college. Niliamua nikaoeleka na yeye ndiye aliniharakisha. Saa hii hakuna wa kuniunga mkono nisome."
Alipopewa fursa ya kumzungumzia mzazi mwenzake hewani, Bi Zainab alisema, "John mimi bado nakupenda. Wewe ndiye ulikuja ukanichukua nyumbani. Mimi bado nakupenda. Wewe ndiye ulikuwa mume wangu wa kwanza."