logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho:Jamaa alia kuachwa na mkewe baada ya mwanamume mwingine kuahidi kumfungulia hoteli

Clinton alisema mkewe aligura ndoa yao ya mwaka mmoja baada ya jamaa kumshawishi aende akamfungulie biashara.

image
na Samuel Maina

Vipindi25 January 2024 - 06:23

Muhtasari


  • •Clinton alisema mkewe aligura ndoa yao ya mwaka mmoja baada ya jamaa kumshawishi aende akamfungulie biashara. 
  • •Clinton alidai mkewe pia alikuwa na mpango wa kumrudia mpenziwe wa zamani aliyekuwa amezaa mtoto mmoja naye.
Ghost na Gidi

Jamaa aliyejitambulisha kama Clinton Nyongesa ,26, kutoka Nakuru alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Vivian Sawinja ,23, ambaye alimtema mapema mwaka uliopita.

Clinton alisema mkewe aligura ndoa yao ya mwaka mmoja baada ya jamaa mwingine kumshawishi aende akamfungulie biashara. 

Pia alidai kwamba mama huyo wa mtoto wake mmoja pia alikuwa na mpango wa kumrudia mpenziwe wa zamani aliyekuwa amezaa mtoto mmoja naye.

"Nilipata anaongea na jamaa fulani kwa simu. Alikuwa jamaa ambaye alikuwa amemwambia aende amfungulie  hoteli wafanye pamoja. Vivian akaanza kujipanga hapo akaondoka akaenda kwa huyo jamaa," Clinton alisimulia.

Aliendelea, "Vivian alikuwa anatumia simu yangu. Alikuwa anatuma picha kwa huyo jamaa. Niliona meseji zao... Sku moja nilikuwa nimeenda sokoni, kurudi nikapata hayuko. Nilipata ameacha mlango na geti wazi. Baadaye niliambiwa ako kwa jirani. Baadaye tena huyo jamaa alikuja na wakaenda na yeye. Nilijariubu kuongea na yeye nimuombe msamaha akaniambia amenisamehea na akasema nimtumie nauli akuje. Nilituma nauli akuje lakini hakuja. Ilifika mahali akaniblock."

Licha ya ku'blockiwa kwenye simu, Clinton alisisitiza angependa kurudiana na mwanadada huyo akisema, "Nilikuwa nimezoea yeye na nilikuwa nampenda. Yeye huwa ananiambia hana mtu lakini najua lienda kwa huyo jamaa."

Pia alizungumza kuhusu jinsi alivyofanya juhudi nyingi za kumshawishi mkewe arudi ila zote zimeangulia patupu.

"Huwa ananiambia nimtumie pesa ya matumizi ya mtoto. Nikishatuma ananiblock," alisema.

Juhudi za kumpatanisha Clinton na Vivian hata hivyo hazikufua dafu kwani mama huyo wa watoto wawili hakupatikana kwenye simu.

Alipopewa fursa ya kumuongelesha mkewe hewani, Clinton alisema, "Tafadhali Vivian nakuomba ukuje tuishi na wewe. Nakupenda kama mke wangu."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved