Jumatano asubuhi, jamaa aliyejitambulisha kama Dickson Ihaji ,27, kutoka Kakamega alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Diana Shiyayo ,23, ambaye alimtema mwishoni mwa mwaka jana.
Dickson alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilisambaratika Disemba mwaka jana baada ya mke wake kuambiwa ana mipango ya kando.
"Tulikuwa tunakaa naye vizuri. Hakuwa mtu wa hasira. Alienda ujombani kwake, kisha akirudi nyumbani kwao.
Kuna mama alimpatia maneno ati niko na wasichana... Vitu mingi tu ambavyo sijafanya. Mimi sielewi," Dickson alisema.
Baada ya kusukumwa na Gidi kusema ukweli, Dickson alikiri kwamba alikuwa na mpango wa kando katika siku za nyuma.
"Ndiyo nimewahi kuwa na mpango wa kando lakini saa hii sina. Ndiyo kulikuwa na msichana. Nimekubali nilikuwa naye na mke wangu akagundua," alisema.
Diana alipopigiwa simu, alibainisha wazi kwamba tayari amemaliza mambo na baba huyo wa mwanawe na kudai kwamba amesonga mbele na maisha yake.
"Msamaha gani na tushamalizana. Sitaki msamaha yake. Hapo hakuna matumaini, sioni," Diana alisema.
Kuhusu madai ya Dickson kuwa na mipango wa kando, alisema, "Hakuna cha kushuku, ni ukweli. Yeye anajua ni wangapi, mimi sijui. Nishamove on."
Dickson alijitetea akisema, "Niliamua kurekebika kwa sababu nampenda sana Diana. Labda ni mpango wa Mungu kama ameamua hivyo."
Diana hata hivyo alisikika kusimama kidete na kushikilia msimamo wake.
"Mimi sitaki. Tushasameheana lakini mambo ya kukaribiana hakuna.Nishaelewa vya kutosha," alisema kabla ya simu kukatika.
Dickson alitoa maelezo zaidi akisema, "Hawakuwa wengi. Huyo msichana anasema ni mmoja. Alikuwa msichana mmoja tu na ni kama alikuwa anamjua juu si wa huko."
Wawili hao hata hivyo hawakuweza kupatana.
Je, ushauri wako ni upi