Jamaa aliyejitambulisha kama Nancy Mumo ,23, kutoka kaunti ya Makueni alituma ujumbe wa Patanisho akiomba kupatanishwa na mume wake Dan Makau ,25, ambaye alikosana naye mapema mwaka uliopita.
Nancy alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilisambaratika Machi mwaka jana kufuatia mizozo ya kinyumbani ambapo mumewe alimfukuza.
"Nimejaribu kuomba msamaha lakini kila mara anasema babake alimwambia atafute bibi mwingine aoe. Kila siku namuomba msamaha turudiane, yeye hataki," Nancy alisema.
Alifichua kwamba alizozana na Dan kuhusu jamaa ambaye alikuwa akimpigia simu sana, jambo ambalo mumewe huyo hakuwa sawa nalo.
"Nilikuwa napigiwa simu sana. Ni rafiki yangu alikuwa ananipigia simu. Tulikuwa marafiki shuleni, alikuwa ananijulia hali tu. Hakuna kitu ilikuwa inaendelea. Nilijaribu kumweleza na akakubali," Nancy alisema.
Aliongeza, "Ilifika mahali akaniambia ashapata dame wa Nairobi hataki madame wa ushago. Mambo yote aliniambia sikuhisi chochote, nilimuelewa. Baadaaye hata mimi nilimwambia niko na kijana fulani. Lakini ilikuwa ni uongo. Nilitaka tuahisi vile nilihisi. Nilitaka nione jinsi ambavyo angefanya."
Dan alipopigiwa simu, alifichua kwamba jamaa ambaye alizozana na mkewe kuhusu alikuwa akimpigia simu mida ya usiku tu.
Alisema mkewe alikuwa akipigia wanaume simu usiku huku wazazi wake wakiskia kwani alikuwa akiishi nyumbani kwao.
"Alisema huyo jamaa nawanga na bibi mchana kwa hivyo hawezi piga mchana. Mimi nilikuwa kazini, yeye alikuwa nyumbani. Nilikuwa napiga simu yake napata ako bize," Dan alisema.
Nancy alimwambia ,"Si uliponiambia uko na msichana wa jijini hutaki wa ushagonilikwambia niko na boy na nikakutumia picha? Haikuwa kweli. Uliniachia mtoto nyumbani, ata hujui mtoto anakula nini. Uko Nairobi unastarehe na wanawake, umeniachia mtoto nyumbani.."
Dan alisema, "Akikushinda nipee nitamlea. Kuna wakati ilifika akawa ananitusi, sikuwahi kumblock. Wacha basi nikublock kama umesema nitakublock."
Nancy alilalamika kwamba mumewe alimfanya aache kazi ili ashughulikie mtoto wao kisha akamtema miezi michache baadaye.
Wawili hao hata hivyo hawakuweza kupatana huku Dan akiahidi kumtafuta mzazi huyo mwenzake baadaye.
Je, ushauri wako ni upi?