Jamaa aliyejitambulisha kama Franco Mukaili Simiyu ,24, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na me wake Sylvia Nasimiyu ,20, ambaye alikosana naye mwishoni mwa mwaka jana.
Franco ambaye ni dereva wa lori alifichua kwamba ndoa yake ya mwaka moja ilisambaratika takriban miezi minne iliyopita baada ya mkewe kumshuku kuwa na uhusiano wa mfanyikazi mwenzake.
"Tulikuwa kwa ndoa kwa mwaka moja. Tulikuwa tumeoana. Kuna madam tulikuwa tunafanya kazi na yeye ambaye alikuwa analeta shida kati yetu," Franco alisimulia.
Aliendelea, "Sylvia alienda kanisa alafu huyo madam akaja kwa nyumba. Wakati huyo madam alivyomuona Sylvia akaanza kunishika shika. Huyo mwanamke alikuwa anataka nimuache Sylvia nimuoe yeye. Na ni mtu ako na familia yake."
Franco alisema tukio hilo lilimfanya mkewe agure ndoa yao na hata kumblock kwenye simu.
"Tuliachana na huyo mpenzi mwingine. Nataka nirudiane na Sylvia kwa sababu naona kuna mambo mengi yanaenda vibaya. Hata mama yangu ananiambia nijaribu kuongea na yeye arudi. Mama akimpigia anamwambia atarudi. Anashika simu ya mama lakini hashiki yangu. Mimi nitangoja mpaka wakati atakuja kunipa majibu. Kufua nguo imekuwa shida kwangu," alisema.
Aliendelea kujitetea, "Makosa ilikuwa yangu. Haikuwa kupenda kwangu. Huyo mwanamke alikuwa anataka kujua mahali nakaa."
Patanisho kati ya Franco hata hiyo iligonga mwamba kwani Bi Sylvia alikata simu na kukataa kushika tena alipopigiwa na Gidi.
"Sylvia naomba urudi kwa nyumba yako. Ni kweli nilikuwa na makosa lakini naomba urudi kwako tuendelee na maisha yetu," Franco alimwambia.
Je, una maoni yapi kuhusu Patanisho ya leo?