Katika kitango cha Patanisho asubuhi kwenye Radio Jambo, mwanadada kwa jina Ruth mwenye umri wa miaka 24 kutoka Kitale alitaka kupatanishwa na mumewe Peter.
Ruth alisema wamekaa kwa ndoa kwa miaka 2 na wana mtoto mmoja na tatizo hilo lilianza Desemba mwaka jana.
Ruth alisema mumewe alimpigia simu akampata ako kwenye simu nyingine na tatizo likaanza hapo ambapo alimkasirikia.
Hata hivyo, bado hawakuwa wameanza kuishi pamoja.
“Alikuwa ananishuku sana, akiona hata nikizungumza na mtu. Alinipata na mtu tukizungumza tu kijamii. Alinipigia simu akapata niko kwenye simu nyingine na hiyo ndio ilileta shida yote. Hatukuwa tumeoana lakini tulikuwa katika mpango wa kuanza kuishi pamoja. Ninataka tu anisamehe kama hiyo simu ilimkwanza, kwani bado mimi nampenda,” Ruth alijieleza.
Peter alipopigiwa simu, alipatikana kwenye kelele sana na hivyo kuifanya vigumu kuwasiliana naye.