Jamaa aliyejitambulisha kama Kelvin Makoha ,29, kutoka Thika alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Zarita ,21, ambaye alikosana naye mwezi uliopita.
Kelvin alisema mkewe aligura ndoa yao ya mwaka mmoja akiwa mjamzito baada ya kushuku ana mipango wa kando.
"Alikuwa ananiushuku niko na wanawake wengine kwa sababu huwa narudi kwa nyumba usiku. Nikamwambia kama ananishuku achukue simu yangu aangalie kama kuna kitu. Lakini ni kama hakuelewa alitoka tu akaenda kwa dada yake," Kelvin alisimulia.
Kelvin hata hivyo alikanusha madai ya kuwa na mahusiano wengini na kueleza kuwa anapenda tu kutangamana na wanawake.
"Mimi napenda kuwa social sana na wanadada. Huwa tunabadilishana mawazo nao, sio maneno ya mapenzi. Huwa nawachukia sana wanaume. Marafiki zangu wote ni wanawake. Napenda kutangamana na wanawake.Wengine huwa wananipea ushauri wa maisha, jinsi naweza kukaa na mke.Sina mahusiano mengine. Nataka kuomba msamaha nataka turudiane tukae pamoja kama kitambo," alisema.
Zarita alipopigiwa simu alibainisha wazi kwamba hana nia ya kurudiana na mpenzi huyo wake.
"Siwezi rudi kwa sasa," alisema Zarita kabla ya simu yake kukatika.
Majaribio ya Gidi kumpata tena Bi Zarita kwa ajili ya kumpatanisha na mpenzi kwa bahati mbaya ziliangulia patupu kwani simu yake ilizimwa.
Kelvin alisema, "Mimi bado nampenda sana huyo msichana. Naomba anisamehe turudiane."
Je, una ushauri upi kwa Kelvin?