logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mke akosana na mumewe aliyempiga mvulana aliyekuwa akimtongoza bintiye

Ilibidi atoroke kwa sababu kundi ya vijana walikuwa wanataka kumpiga na kumkata kata na kisu.

image
na Davis Ojiambo

Vipindi17 April 2024 - 07:36

Muhtasari


  • “Niliwaskia wakiongea maneno machafu nikaenda walikokuwa kukataza kijana huyo lakini akaanza kunitusi na hiyo ilinifanya nimpige.”
Ghost na Gidi

Edward Chemunges kutoka Nandi mwenye umri wa miaka 40 alituma ujumbe akiomba apatanishwe na bibi yake Miriam wa umri wa miaka 35 ambaye walikosana juu ya kumpiga kijana ambaye alikuwa na uhusiano wa mapenzi na binti yake mwenye  ako kidato cha 3.

Chemunges alielezea Gidi na Ghost kuwa alikuwa akiwaskia binti yake na huyo mwanaume wakiongea vitu chafu wakiwa katika chumba kingine na hiyo kilimfanya atoke alipokuwa aende amkataze kijana huyo lakini akaanza kumtusi na hiyo ilimfanya ampige kijana huyo.

“Niliwaskia wakiongea maneno machafu nikaenda walikokuwa kukataza kijana huyo lakini akaanza kunitusi na hiyo ilinifanya nimpige.”

Chemunges aliendeleza kusema baada ya tukio hiyo ilibidi atoroke kwa sababu kundi ya vijana walikuwa wanataka kumpiga na kumkata kata na kisu.

“Baada ya hayo yote ilibidi nitoroke kwasababu kundi la wavulana walikuwa wanata kunikatakata na kunipigi”, Chemunges alieleza kwa uchungu.

Edward aliulizwa kwa nini mambo hao yalifanya mke wake akosane na yeye na alikuwa anajaribu tu kumsaidia binti huyo alieleza kuwa hata yeye mwenyewe haelewi kwa nini imefanyika hivyo.

“Hata mimi sielewi kwanini amekosana na mimi. Alikuwa anakuja mahali nimejificha alafu akaaanza kuacha kukuja, hata nikimpigia hashiki simu zangu na hata hataki kuniona.”

Gidi na ghost walijaribu kumpigia simu Miriam lakini hakushika simu kwa hivyo bado hatuna majibu yake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved