logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa amleta ex wake nyumbani baada ya mkewe kwenda matanga, majirani wamripoti

Humprey alisema ndoa yake ilivurugika mwezi April wakatiex wake alipolala kwake baada ya mkewe kwenda nyumbani.

image
na Samuel Maina

Vipindi09 May 2024 - 06:05

Muhtasari


  • •Humprey alisema ndoa yake ilivurugika mwezi April wakati mpenzi wake wa zamani alipolala kwake baada ya mkewe kwenda nyumbani.
  • •Ivyne alipopigiwa simu hakuwa na mengi ya kusema ila alikubali kumsamehe mumewe.
GHOST NA GIDI STUDIONI

Jamaa aliyejitambulisha kama Humphrey alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Ivyne ambaye alikosana naye mwezi uliopita.

Humprey alisema ndoa yake ilivurugika mwezi April wakati mpenzi wake wa zamani alipolala kwake baada ya mkewe kwenda nyumbani.

"Vile alienda, nilikuwa nimeachana na msichana. Huyo msichana aliniambia anataka kuenda kwao, akauliza kama anaweza kuleta mtoto. Alitaka tukutane mjini aone kama anaweza kuacha mtoto kwangu," Humphrey alisema.

Aliongeza, "Tulikutana mjini akasema anataka akuje nyumbani aone kama mke wangu atakubali aniletee mtoto. Nilimwambia mke wangu hayuko nyumbani akasema anataka twende nyumbani akathibitishe. Tulipofika akapata kweli mke wangu hayuko, akauliza kama anaweza kulala hapo na akaamua kulala. Kesho yake majirani walimuona wakamwambia. Aliniuliza kuhusu hilo nikamueleza, nilimwambia akasema hawezi kurudi hapo tena nimuoe huyo msichana tu. Alikuwa ananiambia tu nichukue huyo bibi nikae na yeye."

Ivyne alipopigiwa simu hakuwa na mengi ya kusema ila alikubali kumsamehe mumewe.

Alithibitisha madai ya mumewe na akasema atarudi kwa ndoa yake kwani tayari aliweza kumsamehe.

"Nitarudi. Nimemsamehea nitarudi," alisema.

Humphrey alisikika kuridhika na uamuzi wa mkewe kumsamehe.

Hajawahi kuniambia atarudi. Na kaka yake nikimpigia anasema nimpee muda," alisema.

Kuhusu uhusiano wake na mama mtoto, alisema, "Siwezi kujua kama mama mtoto ako mtu. Kama anataka mahitaji ya mtoto huwa namtumia. Alisema hataki kusikia maneno kama hayo mradi nishughulikie mtoto."

Je, una maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved