Jamaa ambaye alijitambulisha kama Brian Achochi ,21, kutoka Ruiru alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Sharon Sakwa ,20, ambaye alikosana naye wiki moja iliyopita.
Brian alisema ndoa yake ya miaka miwili ilisambaratika Jumapili wiki iliyopita kufuatia mzozo kuhusu matumizi ya pesa.
"Wiki jana Jumapili, nilimpatia mke wangu kodi ya nyumba. Ilikuwa 3,800. Nikaenda kazini, kurudi kesho yake, nikamuomba hiyo pesa nifanyie kitu fulani ndio niongee na mwenye nyumba akaniambia ametumia. Sikuona kitu alizifanyia hizo pesa, nikamuuliza ametumia aje na hakuna kitu imefanywa kwa nyumba. Hakuniambia ni nini, na rent hakulipa. Nilienda kazini, kurudi jioni nikapata hayuko," Brian alisimulia.
Aliongeza, "Sijajitambulisha kwao lakini nilikuwa nimeambia wazazi wake. Aliniambia atarudi, nikamtumia fare akakula."
Sharon alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba anamtaka mpenziwe kupiga hatua ya kutembea nyumbani kwao.
"Mwenyewe akuje tu nyumbani. Vitu zingine huwa haziongelewi kwa redio," Sharon alisema.
Brian aliendelea kulalamika kuhusu kudanganywa kuwa mkewe anarudi ila bado hajarudi.
"Mbona mamako anidanganye unakuja na hukuji, mpaka nawatumia pesa mnakula? Si ungekuja ama uniambie nikuje nyumbani," alisema.
Kwa upande wake, Sharon alilalamika kuhusu mumewe kumfukuza na kumfungia nje ya nyumba
"Ulinifungia mlango ukanicha nimesimama kama mtu hana kwao... Yeye alitoka akaenda kazi. Akarudi saa moja akapata nafua. Akaniambia anataka niende kwetu. Aliniambia nipange vitu niende nyumbani. Akaniuliza niko na pesa ngapi.Nilimwambia ati niko na mia nne, akasema hawezi kuniongeza nauli niende kwetu. Baada ya siku moja akanitumia 1500 akaniambia nirudi," Sharon alisimulia.
Aliongeza, "Ajilete mwenyewe aone pia mimi niko na wazazi. Aone ile mti aliacha hapo nyumbani haiko."
Brian alisema, "Mimi kwao sitaenda sasa.Mamake pia ni mkora. Mamake alinidanganya ati msichana ako kwa njia, bado hajakuja."
Sharon alisema, "Ndoa ya nairobi sio ndoa, ajilete mwenyewe. Hiyo ilikuwa come we stay. Huku hatuna ubaya, akijileta mwenyewe hakuna mtu ako na ubaya. Mwanaume mzuri ni yule anakuja nyumbani kwenu."
Alisisitiza kwamba Brian anafaa kuenda nyumbani kwao ikiwa anataka kusuluhisha matatizo yao.
Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?