Katika kipindi cha ilikuaje siku ya Jumanne mbunge wa Langata Felix Odiuor anayejulikana kwa jina 'Jalango' alisimulia Maisha yake baada ya kujiunga siasa.
Alisema kuwa baada ya kuingia kwenye siasa akuna jambo ambalo limebadila katika maisha yake.
“Kwa maisha hakuna kitu imebadilika, bado naishi palepale, gari naendesha hile hile na akuna kitu imebadilika hile imebadilika ni wajibu ambao ni mimi napeana suluisho ya matatizo kwa watu lakini kwa mtindo wa Maisha akuna ambacho kimebadilika maisha yangu yanaendelea kama ilivyokua kitambo” alisema.
Alieleza kuwa anafurahia sana Maisha ya siasa kwa sababu anatumikia watu ambao walimtuma mbungeni kuwafanyia kazi.
“Nafurahia sana sana ninacho furahia zaidi ni kufanya kazi na watu wanakwambia asante, ni raha sana wakati watu wanakwambia hawana maji katika eneo lao unafanya bidii wanapata maji na kutengeneza barabara ni raha sana na baadae wanakwambia asante.”
Alisema kuwa kwa uchanguzi ujao atakua bado anawania kiti cha ubunge Langata na kulingana na vile amefanyia watu wa Langata kazi anamatumahini kua atashinda tena.
Alipoulizwa kutokee akose kupata kiti cha ubunge wa Langata katika uchanguzi ujao alisema sio lazima arejee katika utangazaji.
“Bona nirundi utangazaji si lazima nirundi utangazaji naeza rundi kufanya biashara zangu ama bado nirundi utangazaji lakini mbona nisirundi siasa na ukifanyia wananchi kazi utapata kura,” Jalango alisema.