Katika kitengo cha Patanisho, jamaa aliyejitambulisha kama Simon Juma ,30, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Cynthia Achieng ,24, ambaye alikosana naye mwezi uliopita.
Juma alisema ndoa yake ya miaka nane ilivunjika mwezi jana kufuatia mzozo wa kinyumbani uliopelekea mkewe kutoroka.
"Tulikosana kwa nyumba na nikampiga. Tulikaa karibu wiki mbili hivi akaenda nyumbani. Alienda na watoto wawili akaacha mmoja mkubwa. Nilimpiga kwa sababu ya hasira. Sijui ni shetani ama ni nini," Juma alisema.
Aliongeza, "Tulikuwa tunaongea hapo nyuma nyuma lakini sasa hatuongei. Nikimwandikia meseji anajibu na matusi."
Cynthia alipopigiwa simu, alibainisha kwamba mzazi huyo mwenzake ndiye aliyemfukuza kutoka nyumbani kwao.
Aidha alifunguka kuhusu meseji mbaya ambazo Juma alikuwa akimtumia, ambazo zilimfanya hadi abadilishe namba.
"Ata nimeshangaa ananitafuta! Mwenyewe aliniambia nipange vyangu niende mahali nataka kuenda. Nilishangaa ananitafutia nini. Nilibadilisha hata namba akafanya bidii akapata yangu mpaya. Sikuwa nataka kuongea naye kulingana na vile alikuwa ananitumia meseji mbayambaya nikiwa kwetu hadi nikadadilisha namba," Cynthia alisema.
Juma alichukua fursa hiyo kuomba msamaha na kumsihi mkewe arudi ili waendelee kulea watoto wao watatu.
Cynthia alimwambia, "Nilikwambia endelea na maisha ya.Ulisema unataka mkamba mzuri mwenye kifua chake kimesimama juu changu kimelala. Wewe tafuta tu huyo Mkamba."
Juma alisema, "Kuna kitu alinifanyia ambayo siwezi kuongea kwa redio."
"Yeye aendelee na maisha yake. Hakuna muda naweza kumpea kwa sababu hata nikirudi bado atarudia. Mara ya kwanza tulikosana akanikujia kwetu. Alisema nimejilazimisha kwake. Sasa ata nikirudi si atasema nimejilazimisha kwake. Tunakosania mambo tu ya nyumba.
Alisema ataniendea kwa mganga aniulie watoto. Alisema nisipeleke watoto kwetu ataniendea kwa mganga . Ata mimi alisema ataniendea kwa waganga nikuwe wazimu nianze kuokota vitu mjini," Cynthia alisema.
Juma alimwambia, "Apoe roho yake arudi tulee watoto. Hiyo ya waganga ni kushtua tu. Aki darling nakuomba urudi tu. Hiyo mambo yote tusameheane turudi vile tulikuwa. Mtoto anauliza mama ako wapi, namwambia mama atarudi."
Hata hivyo, hakuwa na budi ila kukubali uamuzi wa mzazi huyo mwenzake.
"Aendelee na mkamba mwenye matiti zake zimesimama," Cynthia alisema.
Je, ushauri ama maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?