Jamaa anayejulikana kama David,24 kutoka Eldoret alituma ujumbe akitaka kupatanishwa na mpenzi wake Sylvia mwenye umri wa miaka 24 baada ya kukosana Mei ,2022.
David alisema kuwa alikosana na Sylvia kwa sababu ya ulevi na wamekuwa kwa mahusiano kwa takriban mwaka moja.
"Tulikaa na Sylivia kama miezi sita ,baada ya hapo nikamchukua tuishi naye,nikaanza kunywa pombe na hivo tukakosana akaenda kwao.Huwa tunaongea na yeye lakini si sana vile.Mimi naamini ni pombe maana sijawahi mkosea.Huwa namtukana saa zingine akikataa kushika simu,ila tukiishi na yeye sikuwa namtusi...'
Aliongeza,"Huwa naenda kwao ,Januari mwaka huu nimeenda kwao lakini nilipofika niliambiwa ameenda kazi..."
David alikiri kuwa kwa sasa aliacha pombe na yupo tayari kujibadilisha na kusonga hatua ya mbele ya maisha.
Sylvia alipopigiwa simu alidai kuwa David alikuwa na ujinga na alikuwa amemwambia awachane na yeye.Sylivia alidai kuwa yeye yuko sawa na hamhitaji David.
"Huyo jamaa alinikataza alimove on,mimi nashughulika na hustle yangu huku...simtaki.Aliniandikia messages mbaya mbaya ,sina mtu lakini nilimsahau.Mimi sijui nilkosea wapi..."
Sylivia alisisitiza ,'Nimempea chance almost mwaka moja na nusu lakini sioni akirekebisha tabia zake..."
Alipoulizwa kuhusu shida ya David,alisema; 'Shida yake kubwa ni kama ni 'utotology' [Akicheka] si mtu amekomaa kiakili,yeye hueka mzaha kwa kila jambo anapoongea.Mimi nikimkubali nilidhania labda atanichukua aniweke tuanze maisha yetu pamoja...yeye hueka wasichana wengine kwa mitandao ya kijamii na kuniambia kuwa anafanya hivo ili nikasirike na iniumize roho..."
David alikubali makosa yote na kusema kuwa yupo tayari ila pia alisisitiza kuwa Sylvia alikuwa anasema ubaya wake na wala si mazuri ambayo ametenda .Hata hivyo David aliongeza"Nakutakia maisha mazuri,nitakupa muda jinsi ulivyosema na ninakuombea dua kila siku,lakini yafaa ujuwe nakupenda sana..."
Sylvia kwa upande wake alisema "Kama atakuwa 'amegrow up' na afahamu ni nini anataka kwa maisha basi anitafute..."
Je,una maoni gani kwa patanisho ya leo?