logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho:Jamaa asamehewa na mamake kwa kutomsaidia

Anos alikosana na mama yake tangu mwaka wa 2020 kwa madai ya kutomsaidaia kimaisha.

image
na Davis Ojiambo

Vipindi27 June 2024 - 06:40

Muhtasari


  • •Anos alisema kuwa alikosana na mama yake tangu mwaka wa 2020 baada ya kukisia kuwa hakuwa anamsaidia katika hali ya maisha.
  • •Mamake Anos alipopigiwa simu alimsamehe huku akimwomba kijana kutorudia makosa ya uongoo baada ya kudai kuwa alikuwa anamsaidia kwa chama.

Jamaa mmoja anayejulikana kama Anos Ochieng alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mama yake anayefahamika kama Sylvia kutoka Kakamega baada ya kukosana tangu 2020.

Anos alisema kuwa alikosana na mama yake baada ya mama yake kuteta kila mara eti hamsaidii kimaisha na kudai kuwa kila mara wakikutana hawaelewani.

'"Nilitoka nyumbani mwaka wa  2020 ,kwa sasa nipo Nairobi.Nilikuwa nasaidia mama ,kila baada ya mwezi nilikuwa namtumia mama shilingi elfu moja.Pia nilikuwa namsaidia kuchangia chama.Hatuelewani vizuri kwa sasa ,kila ninapompigia simu,hunigombanisha kila wakati,huku akitaka nimtumie pesa kila siku..."

Anos alisema kuwa alikuwa na dada ambaye pia yupo Nairobi na anafanya kazi akidai kuwa dada yake pia humsaidia mama.Hata hivyo,Enos alisema kuwa mama yake yupo kwao na wala si kwa bwanake [babake Enos] .Tangu akiwa mtoto hajawahi kumwona babake.

"Sijawahi kutana na baba yangu..."Anos aliseama .

Mamake Anos alipopigiwa simu alisema kuwa yeye hana shida yoyote na Enos na haoni kama Anos alitenda mabaya yoyote.

"Mimi sina chuki yoyote na  Anos, kwa sababu mimi naelewa hali ya watoto na mimi ni mama mlezi.Ninaelewa mtoto anapokosea mahali,nikijaribu kufikiria kuona kuna utatanishi wowote mimi hupiga chini magoti na kuomba .Nimekuwa nikiombea kijana yangu na sina ubaya wowote na mwanangu.Ninampenda kijana yangu,ni kijana yangu mmoja pekee."

Hata hivyo,mamake Sylvia alikanusha madai ya Anos ya kumtumia pesa kila mwezi akitsema kuwa Anos alikuwa akidanganya .

"Kwa upande wangu mimi nimeokoka na sipendi uongo,hadi huyo kijana yangu anajua nimeokoka na sipendi uongo.Huwa hanitumii kila siku ama kwa mwezi.Hapo amedanganya.Hadi kwa chama niliamua kujitoa kwa sababu sina uwezo wa kulipa..."

Hata hivyo Sylivia alimwomba kijana yake kutorudia makosa ya uongoo baada ya kuomba msamaha.

Je,una maoni gani kwa patanisho ya leo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved