Jamaa aliyejitambulisha kama Shaban Sale ,34, kutoka Mumias alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Faiza Shaban ,30, ambaye alikosana naye hivi majuzi.
Shaban alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilisambaratika wiki jana baada ya yeye kushinda akimshinikiza mkewe amzalie mtoto.
"Nimekaa naye miaka mingi lakini hanipi watoto. Hazai. Tulienda kwa daktari tukapewa dawa tukatumia lakini hakuna matokeo. Tayari miaka mitatu imeisha. Sasa ametoka akaenda kwao," Shaban alisema.
Aliongeza, "Nilikuja kwa nyumba nikamwambia, hii nyumba tutaishi hivi bila mtoto. Ni vile tu nilikuwa na hasira ya kutaka mtoto. Nashuku yeye ndiye ako na shida. Amekuwa akitumia dawa za kupanga familia sana. Mimi niko sawa. Nimekuwa na warembo kadhaa, na kumekuwa na kesi za kupeana mimba nje, niko na watoto wawili nje, mama zao walikwamilia watoto. Muda unaenda, anafaa aangazie mambo ya watoto. Watu wa kwao wananiambia niwe mpole. Nilitaka kujua uamuzi wake."
Faiza lipopigiwa simu alipinga kuwa yeye ndiye mwenye tatizo na kubainisha kwamba yeye tayari ana watoto wawili.
"Ananilaumu mimi, na mimi niko na watoto wawili, yeye hajawahi kupata. Watoto sio wake, anajua. Anasema mimi nilienda kwa family planning niliua mayai yote kwa tumbo. Shida ni yeye. Yeye hana watoto," Faiza alisema.
Shaban alitetea kwa kusema; "Pia mimi niko na watoto lakini huwa sikwambii kwa sababu nakuheshimu. Wakati tuliachana na wale warembo wa kitambo walikuja nyumbani wakaambia mama wako na watoto wangu. Ni wangu lakini mama zao ndio wanajua zaidi. Mimi najua niko sawa."
Faiza hata hivyo alisisitiza kwamba yeye hana tatizo na akamtaka mpenziwe huyo atafute mwanamke mwingine.
"Nilikwambia mwenye anakuzalia, ulisema mimi sizaangi. Ulisema unataka kuenda Nairobi kutafuta mtu.. Ata wazazi wake waliniambia hana mtoto nje. Aende arudishe mwenye alizaa na yeye, aendelee kumzalia. Mambo yake sitaki," alisema.
Shaban kwa kumalizia alisema, "Kama ameamua ni sawa, yeye ndiye mwenye uamuzi. Mimi nilikuwa nampenda sana, kama ameamua hivyo ni sawa."
Faiza akasema, "Atafute mwanamke wakae maisha mazuri. Nimeamua nikae tu pelee yangu. Sitaki kwa sasa kuingia kwa mambo ya ndoa. Mi najua niko sawa, najua tumejaribu hatujafanikiwa."