logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Huyo simjui!" Mwanadada amkana mumewe baada ya kumtumia pesa 'zisizotosha'

"Huyo simjui. Mimi simjui!" alisema kabla ya kukata simu.

image
na Samuel Maina

Vipindi09 August 2024 - 06:20

Muhtasari


  • •Bosire alisema ndoa yake ya miaka saba ilisambaratika siku tatu zilizopita baada ya mke wake kutoridhika na fedha alizomtumia.
  • •Bi Kerubo alipopigiwa simu hata hivyo alimkana mzazi huyo mwenzake na kubainisha kwamba hamjui.

Katika kitengo cha Patanisho, Bernard Bosire (42) kutoka kaunti ya Kisii alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Lydia Kerubo (32) ambaye alikosana naye hivi majuzi kuhusiana na masuala ya kifedha.

Bosire alisema ndoa yake ya miaka saba ilisambaratika siku tatu zilizopita baada ya mke wake kutoridhika na fedha alizomtumia.

"Yeye ako nyumbani, mimi nafanya kazi Kisii. Juzi alafu nikamtumia pesa ingine hapo, akaona kama ni kidogo. Ndio nilikuwa nimeanza kazi, nikalipwa nusu. Nilimpigia simu mara tatu, akakataa kushika. Baadaye alishika akaanza kuniongelesha vibaya. Nilijaribu kumueleza lakini hatukuelewana," Bosire alisema.

Alisisitiza kwamba kabla ya kuanza kazi yake mpya, alikuwa akiwajibika na kushughulikia majukumu yote ya nyumbani.

Bi Kerubo alipopigiwa simu hata hivyo alimkana mzazi huyo mwenzake na kubainisha kwamba hamjui.

"Huyo simjui. Mimi simjui!" alisema kabla ya kukata simu.

Bosire alipopewa nafasi ya kuzungumza naye hewani, alimwambia, "Mama Jane, mimi nakupenda. Na sitaki tena upotee. Urudi kwa ndoa tukae kwa amani."

Je, ushauri ama maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved