logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gidi azungumzia jamaa wa Equatorial Guinea aliyeshiriki mapenzi na wanawake 400, ashangaa jinsi waume zao hawakuwahi kujua

Gidi alihitimisha kuwa wanawake wanajua kuficha mambo yao kuliko wanaume.

image
na Samuel Mainajournalist

Vipindi07 November 2024 - 09:32

Muhtasari


  •  Gidi alishangaa jinsi wapenzi wa mamia ya wanawake wanaodaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Bw Engonga hakuwahi kupata kuvumbua kwamba wake zao walikuwa wakitoka nje ya ndoa.
  • Gidi alibainisha kuwa si rahisi kwa wanaume kujua wake zao wanatoka nje ya ndoa.



Katika kitengo cha Maoni ya Patanisho siku ya Alhamisi, mtangazaji wa kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi Gidi Ogidi alibua mjadala kuhusu jinsi mtu anaweza kubaini ikiwa mpenzi wake anacheza karata nje ya ndoa ama mahusiano.

Mjadala huyo ulitokana na Patanisho ya Alhamisi asubuhi iliyogonga mwamba ambapo Kelvin Chege alitaka kupatanishwa na mpenzi wake Mercy Cheruiyot ambaye alimuacha baada ya kumshuku kuwa na mipango ya kando.

“Mjadala wa leo, ningependa kupatia wanadada na wanaume nafasi, uniambie ni njia gani huwa unaangazia kuweza kujua kama mpenzi wako anafanya udanganyifu,” Gidi alisema.

Mtangazaji huyo mahiri alibainisha kwamba aghalabu wanaume wanapopatikana wakijihusisha na mahusiano ya kando huwa wanastaajabishwa na jinsi wapenzi wao walifanikiwa kuwavumbua.

“Mara nyingi wanaume wanashangaa, alijuaje? Huwa wanashanga wapenzi wao ama wake zao walijuaje. Wanadada nao pia mambo yao huwa ngumu sana kujua,” alisema.

Gidi pia alitumia fursa hiyo kuzungumza kuhusu kisa chenye utata cha hivi majuzi ambacho kinahusu mwanaume mmoja wa Equatorial Guinea anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake zaidi ya 400 walioolewa.

Mtangazaji huyo wa kipindi cha asubuhi alishangaa jinsi wapenzi wa mamia ya wanawake wanaodaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Bw Baltasar Ebang Engonga hakuwahi kupata kuvumbua kwamba wake zao walikuwa wakitoka nje ya ndoa zao.

“Kuna jamaa mapenzi na mabibi za hata wakuu wa jeshi, na mamlaka wa serikali. Yaani unataka kuniambia hawa wanaume hawakuweza kujua kwamba wake zao wanakwenda kando kando ya ndoa? Iligunduliwa tu baada ya zile video ambazo huyu jamaa alikuwa anarekodi kufichuliwa!!” Gidi alisema.

Mwimbaji huyo wa zamani wa kundi la Gidi Gidi Maji Maji alihitimisha kuwa wanawake wanajua kuficha mambo yao kuliko wanaume.

“Ningependa kujua siku ya leo, ni dalili gani ukiona bwanako unajua huyu ameanza kudanganya, ili wengine waweze kujua,” alitangaza.

Aidha, alibainisha kuwa moja ya njia wanazotumia wanawake kujua waume zao wanaenda nje ya ndoa ni pale wanaporudi nyumbani jioni wakinuka harufu ya manukato ilhali wanaume wengi wanajulikana kuoga mara moja tu asubuhi.

Pia alibainisha kuwa si rahisi kwa wanaume kujua wake zao wanatoka nje ya ndoa.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved