logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Hafla ya mahari iliyopangwa kufanyika kesho, harusi ya Disemba hatarini baada ya bibi harusi akim'block bwanake

Collins alisema wamepanga safari ya kwenda kwa kina Njoki kutoa mahari siku ya Jumamosi ila mpenziwe huyo hajakuwa akishika simu zake.

image
na Samuel Mainajournalist

Vipindi08 November 2024 - 08:50

Muhtasari


  • "Kuna wakati alikuwa mjamzito, sijui nini ilifanyika akaenda akatoa mimba. Hadi nilikuwa nimeambia hata wazazi wangu," Collins alisema.
  • Collins alieleza wasiwasi wake huku akifichua kwamba alipanga kuenda kutoa mahari siku ya Jumamosi.


Collins Shikuku 30yrs kutoka Kakamega, please naomba munipatanishe na Mchumba wangu Eunice Njoki 26yrs. Tumekuwa kwa uhusiano kwa miaka miwili na tulikuwa tumepanga kufunga ndoa mwezi wa December 2024. Nilikosana na yeye juzi na communication yetu haijakuwa nzuri, nikimuuliza ni nini anakuwa kali.

Jamaa aliyejitambulisha kama Collins Shikuku ,30, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Eunice Njoki ,26, ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Collins alisema uhusiano wake wa miaka miwili uliharibika siku chache zilizopita baada ya Njoki kugeuka ghafla na kuwa mkali kwake.

Alisema walipanga kufunga ndoa mwezi ujao ila mambo yanaonekana kuenda vibaya kwa sasa.

 "Tulikuwa tunapanga kuoana mwezi ujao. Jumatatu wiki hii alinipigia simu akaniambia anataka Kwenda saluni nimtumie pesa. Sikuwa na pesa ambazo alikuwa anataka. Nikamtumia zenye nilikuwa nazo. Tumezoea akienda saluni ananitumia picha ya vile ametengenezwa nywele. Aliniuliza kwani ni lazima anitumie picha. Hapo ndo alikasirika, nikimpigia simu anakuwa mkali. Jana ndio aliniweka blacklist. Dadake aliniambie ako nyumbani lakini hajamueleza shida ni nini. Mimi sijamkosea, labda yeye aeleze," Collins alisimulia.

Pia alizungumza kuhusu tukio lingine la kuibua wasiwasi katika mahusiano yake ambapo mchumba wake alitoa mimba.

"Kuna wakati alikuwa mjamzito, sijui nini ilifanyika akaenda akatoa mimba. Nilikuwa nimeambia hata wazazi wangu. Mwishowe akawa ametoa hiyo mimba, mama yangu alikasirika na pia mimi nilikasirika. Alikuja tukaongea na tukamaliza nikakubali tuendelee," alisema.

Jaribio la kuwapatanisha wawili hao kwa bahati mbaya halikufua dafu kwani Njeri alikataa kuzungumza kwenye simu.

Collins aliendelea kufunguka kuhusu hali ya mahusiano yake na kueleza wasiwasi wake huku akifichua kwamba alipanga kuenda kutoa mahari siku ya Jumamosi.

"Nilikuwa nimepanga safari kwenda kupeleka mahari kesho. Kuna watu nishaambia wanajua safari ni kesho. Kwa sasa Njoki ameniweka blacklist. Sijaambia wazazi kwamba safari haitakuwa. Hashiki ata simu zangu," Collins alisema.

Gidi alimshauri Collins ajaribu kumpigia mpenziwe ili aone kama wataweza kusuluhisha mzozo wao pamoja.

Je, ushauri wako kuhusu Patanisho ya leo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved