logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa amfukuza mkewe mjamzito kwa kuvunja kifuli ya nyumba, amwambia asahau mambo ya ndoa

"Mke wangu mgani? Mke wangu niko naye hapa, kwani niko na mwingine nje?" Patrick alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Vipindi14 November 2024 - 08:39

Muhtasari


  • Dorcas alisema ndoa yake ya chini ya mwaka mmoja ilisambaratika Juni 2024 baada ya yeye kuvunja kifuli ya nyumba yao jijini Nairobi.
  • Patrick alipopigiwa simu, aliruka Dorcas kuwa mkewe na akadai kwamba ana mke kwa nyumba.


Dorcas Nekesa ,22, kutoka Kakamega alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Patrick James ,24, ambaye alikosana naye takriban miezi mitano iliyopita.

Dorcas alisema ndoa yake ya chini ya mwaka mmoja ilisambaratika Juni 2024 baada ya yeye kuvunja kifuli ya nyumba yao jijini Nairobi.

"Tulikuwa tunaishi pamoja, nilikuwa nimeenda kuona mama nyumbani. Nilimaliza wiki moja. Sikumwambia narudi Nairobi wakati nikitoka nyumbani. Nilipofika Nairobi, nilienda kwa nyumba sikumpata, nikavunja padlock. Aliporudi alikasirika, akanipa adhabu ya kuenda nyumbani kwa wiki moja. Aliniadhibu kwa kuvunja kifuli," Dorcas alisema.

Aliongeza, "Nilirudi nikakaa wiki moja, kisha akanitumia nauli nikarudi Nairobi. Tulikaakaa hatukuwa tunakaa vizuri, akanikataza kuongea ma msichana fulani jirani, mimi nikawa kichwa ngumu sikusikiliza. Akaniambia nirudi ushago tena. Sasa hivi niko ushago kwetu. Huwa ananipigia simu, nikimuuliza stori za kurudi ananikasirikia. Hatuna mtoto, ndio niko na mimba. Nikimuuliza mambo na kliniki ananitumia pesa. Ningetaka kurudi Nairobi." 

Patrick alipopigiwa simu, aliruka Dorcas kuwa mkewe na akadai kwamba ana mke kwa nyumba.

Hata hivyo, alikiri kwamba Dorcas ana ujauzito wake na akabainisha kwamba yuko tayari kusaidia masuala ya mtoto.

"Mke wangu mgani? Mke wangu niko naye hapa, kwani niko na mwingine nje?" Patrick alisema.

"Huyo msichana akwambie kitu inaeleweka aache kuharibu saa. .Amenitumia meseji nikamtumia usaidizi alikuwa anataka. Nilishamwambia tuongee kwa usaidizi wa mtoto lakini tusiongee mambo ya bibi na bwana. Hiyo apana. Tayari niko na bibi," aliongeza.

Patrick alifichua zaidi, "Alituma meseji eti tumbo inamsumbua akasema nimtumie pesa aende atibiwe. Stori mingi sitaki, kama ako na shida ingine atume simu atasaidiwa. Amesema eti hawezi kuamka, anataka aende asuguliwe. Nimemtumia pesa aende ashughulikiwe? Nini ingine anataka? Mimi sio daktari, nishamuwekea kitu alikuwa anataka . Mambo ya ndoa atoe akilini, na matusi atoe, akileta stori mingi mimi naacha."

Patrick alisisitiza kwamba Dorcas ndiye mwenye makosa na akabainisha kwamba haeleweki.

"Sijamrusha, anajua makosa yake. Leo mtaongea na yeye akuelewe, kesho kichwa imeruka. Siku ingine anakuja kuomba msamaha, mtu kama huyo mtakaa aje na yeye? Shida ni eti huyo msichana haeleweki. Yeye anaingia kwa watu wako na nyumba zao, wanamharibia boma. Usaidizi wa mtoto atapata yote, lakini kuishi naye itakuwa ngumu," alisema.

Dorcas alisema, "Alikuwa ameniahidi atanioa. Kama ameamua hivyo, sina budi, itabidi nikubali tu."

Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved