BAADA ya miezi kadhaa ya kuwapa furaha watumizi wa Android, program ya Songa Play sasa imetanua mbawa za huduma zake za burudani hadi kwenye iOS, kama njia moja ya kuwajali watumizi wa vifaa vya Apple pia.
Songa Play, ambalo ni jukwaa la kipekee linalokupa
burudani ya vipindi vyote vya Radio Jambo na muziki kwa saa 24 kila siku, sasa
linaweza pakuliwa si tu kupitia PlayStore lakini pia kwenye IOS.
Hili ni jukwaa la kidijitali lililobuniwa na shirika
la Habari la Radio Afrika ili kuwajali mashabiki wa vipindi vyote vya Radio
Jambo.
Uzuri wa kuwa na Songa Play kwenye simu yako, unaweza
kufuatilia vipindi pendwa kama vile Patanisho ya Gidi na Ghost, DeadBeat ya
Massawe Japanni, Toboa Siri na Mbusii na Lion miongoni mwa vipindi vingine,
popote na muda wowote.
Jukwaa hilo lilizinduliwa takribani miezi 5 iliyopita
kwa watumizi wa vifaa vya Android, lakini sasa linafurahia kutaarifu umma
kwamba hata wale wanaotumia vifaa vya Apple wanaweza kufurahia vipindi vya
Radio Jambo na muziki kwa kupakua program hiyo ambayo sasa inapatikana kwenye
IOS.
Stesheni zote, zikiwemo Radio Jambo, Kiss 100 FM, Classic
105, Gukena FM, Home Boyz na East FM zina vipindi vyao vyote katika jukwaa la
Songa Play ambavyo vinapeperushwa kwa saa 24 kila siku.
Vipindi hivyo ni pamoja na podkasti pendwa zinazoifanya
stesheni ya Radio Jambo kupepea na kutawala mawimbi ya utangazaji Kenya kwa
zaidi ya miaka kumi iliyopita.
Kama una simu yako ya mkononi, iwe Android au iPhone, sasa
unaweza ukajumuika na mamilioni ya watu wanaopata burudani lisilo na kikomo kwa
kujisajili bila malipo kwenye Songa Play kupitia www.songaplay.com au kupakua program kupitia
Play Store au IOS.