Akizungumza wakati
wa kipindi cha Jumanne asubuhi, kocha huyo wa zamani wa Harambee Stars
alifichua kuwa kisa hicho kilitokea katika msimu wa Valentines uliopita.
Ghost alisimulia jinsi alivyoitisha mkutano wa familia mnamo siku ya wapendanao, bila kujua kwamba wanawe wenye umri wa zaidi ya miaka 18 walikuwa na mipango yao wenyewe pamoja na mpenzi wao.
“Kuna siku nimewaambia vijana wangu kitu, na pia mimi nikajiona nilikuwa labda tu fala. Kuna siku ya Valentine fulani niliwapigia simu nikawaambia ‘Kesho tunaenda Valentine kama familia’. Wakanyamaza, kesho yake wakaniandikia barua wakaniambia, ‘Baba, si uko na mpenzi wako, mama yetu, mpeleke yeye, pia sisi tuna wapenzi. Wewe tupatie tu pesa pia sisi tukajishughulikie, uliona wapi Valentine ya familia kama mtu amefikisha miaka 18?” Ghost alisimulia.
Mtangazaji huyo mahiri wa redio alikiri kwamba tukio hilo lilimwacha akiwa na aibu lakini hakuwa na budi ila kuheshimu maamuzi ya wanawe.
Ghost alitumia fursa hiyo kuwasihi wazazi wengine kuwa wanawaelewa watoto wao na daima kuheshimu maamuzi yao binafsi.
“Nilijiona fala sana, sasa kutoka hiyo siku huwa nawauliza wako na mpango gani. Huwa nawauliza kama wanapatikana,” alisema.
“Kama mzazi, lazima uelewe kwamba kila mtoto wako na utu wake. Lazima ujue kwamba huwezi kuwasimamia watoto wako tena wakishafikisha miaka 18. Mimi niliwaambia baada ya kufikisha miaka 18, wajue kwamba wao ni watoto wa serikali.
Wazazi wanafaa kuwa wanafahamu watoto wao, na watoto pia wafahamu wazazi wao. Hata kwa Bibilia, wazazi walikuwa wananakosana na watoto wao na pia watoto wanakosana na wazazi. Cha muhimu ni kuwe na heshima,” aliongeza.
Akizungumzia yaliyompata mtangazaji mwenzake, Gidi alimweleza kuwa alichokifanya ni cha aibu kwa kweli.
“Wewe Mulee pia wewe ulichoma bana, unachunga vijana wa miaka 18 unataka kuwapeleka Valentine na wako na wapenzi?,” Gidi alimwambia mwenzake.
Ghost
aliweka wazi kuwa sasa anaelewa haiba ya watoto wake kutokana na kutokana na
kutembea sana.
"Kwa sababu ya exposure, vijana wangu, kila mtu namelewa, najua personality yake," alisema.