Baba yangu alikataa kunisomesha, sikujua kama nitaweza kujiunga na chuo kikuu-Mutumishi

Muhtasari
  • Nilifanya kazi ya uhalifu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu Mtumishi aeleza safari ya maisha yake
  • Mchekeshaji huyo alifanya kazi ya uhalifu kwa mwaka mmoja na nusu
Mutumishi

Leo hii katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye mcheshi Gilbert Barasa almaarufu Mutumishi kwenye sudia zetu huku akieleza jinsi amekua.

"Nilikuwa na miaka sita, baba alitoka na kuacha familia yetu, alituacha na mama, baada ya kufika kidato cha pili mama alifutwa kazi na kutuambia tuende kwa baba yetu

Tulipofika kwa baba yetu aliniambia hawezi nisomesha na mimi na ndugu zangu tunapaswa kuondoka na turudi kwa mama yangu, ilhali mama alikuwa amerudi mashambani." Alieleza Mutumishi.

Mutumishi baada ya kuhangaika mitaani alijiunga na kikundi cha uhalifu ambapo aliponea.

"Tulikuwa tu tunafuata maagizo ya mkubwa wetu ya kuiba pesa, tuliposhikwa tuliambiwa tunapaswa kuenda nyumbani na kubadilika, tulipewa nauli lakini sikuenda nyumbani nilienda Mombasa

Nilirudi tena Nairobi na nikapatana na mwanamke ambaye alinisaidia nilimuambia nataka kurudi shule hapo nilirudi shule nikamaliza kidato cha nne na kisha nikajiunga na chuo kikuu

Kwa mawazo yangu sikujua kama nitajiunga na chuo kikuu." Alisema Mutumishi.

Mchekeshaji huyo alifichua kuwa mama yake hakuunga mkono ndoto zake za ucheshi maanake alikuwa nasema kwamba anamwaibisha.

"Niliacha kazi ya kunyoa maiti baada ya rafiki yangu kuletwa akiwa amechapwa na Wananchi kwa ajili ya wizi

Baada ya muda nianza kuota ndoto mbaya kwa maana sikuwa  nimezoea."

mutumishi

Mutumishi alifichua kuwa Daniel Ndambuki ndiye alifanya ampate mkewe walipokuwa kwenye mkutano Nakuru.

Kwa mengi zaidi tembelea youtube ya Radiojambo.