Kuna wakati ilifika nikachukia jina langu - Njoro the comedian adai

Muhtasari

Mchekesjai Njoro alifichua kuwa aliharibu pesa zake alizotoka nazo marekani kwa raha na wanawake

Pia alisema kwamba anajutia kwa vitendo ambavyo alikuwa anafanya 

Njoro
Njoro

Leo hii katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye mchekeshaji Njoro the Comedian ambaye alieleza jinsi alipata msongo wa mawazo.

Kabla ya kupatwa na msongo wa mawazo alienda kufanya kazi marekani na kisha kurudi humu nchini.

"Nilipotoka marekani nilikuwa na pesa nyingi lakini nilitumia pesa hizo kwa raha na kulipa madeni, nilipata msongo wa mawazo kwa ajili ya shinikizo kutoka kwa watu na familia

Nilianza kukunywa vibaya nilikuwa narudi nyumbani saa tisa usiku na kisha naenda kukunywa saa kumi na moja

Sikujali watoto walikuwa wanakula nini wala kuvaa nini, bibi yangu alichoka na kuniacha kusema kweli mke wangu hangeishi maisha ambayo nilikuwa naishi." Njoro Alieleza.

Miezi mitatu iliyopita mcheshi wa Churchill Zainab alifichua kuwa mchekeshaji mwenzake amerudi na nyumba huku wakimpeleka katika shule ya marekebisho.

Akiwa kwenye mahojiano Njoro alisema kwamba msanii Jimmy Gait alimsaidia sana wakati alipohitaji msaada.

"Kuna wakati ulifika nikachukia jina la njoro the comedian kwa maana nilihisi ndilo limeniletea shida hizi zote,wakati nipokuwa na msongo wa mawazo marafiki wengi walinikimbia

Nakumbuka kunawakati mkono wangu haungesonga." Alisema.

Njoro alisema kwamba wakati ke wake alienda mambo ndio yalikuwa magumu zaidi kwa maana alikuwa anabugia vileo kwa sana ilhali hakuwa anakula.

"Nilipokuwa nakunywa nilikuwa natumia kondomu kufanya ngono kwa maana ukiwa mlevi sikuwa najielewa nilikuwa naficha kwa gari

Hiyo ndio ilichangia mke wangu kuenda kwa maana alikuwa anazipata kwa gari, nimerudi katika kazi ya uchekeshaji nangoja corona iishe nirudi."

Huku akizungumzia jinsi watu na wanamitandao wanamlaumu Daniel Ndambuki almaarufu Churchill alikuwa na haya ya kusema

"Watu wanamlaumu churchill bure."

Kwa mengi zaidi tembelea radiojambo youtube.