logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Heshima ni muhimu kuliko pesa kwangu,' Mejja aeleza kwa nini alikataa collabo na WCB

Mwaka jana Mejja alivuma sana baada ya kukataa collabo na lebo ya WCB

image
na Radio Jambo

Habari11 January 2021 - 10:38

Muhtasari


  • Mejja aeleza kwanini alikataa collabo na WCB 
  • Msanii huyo alidai kwamba anatambua heshima katika maisha yake kuliko pesa
  • Pia alisema kwamba amekuzwa na mama pekeyake huku akipitia changamoto tofauti

Leo hii studioni tulikuwa naye msanii na rappa Mejja ambaye alizungumzia mambo kadha wa kadha na jinsi kama msanii anaishi maisha yake.

Mwaka jana Mejja alivuma sana baada ya kukataa collabo na lebo ya WCB inayomilikiwa na staaa wa bongo Diamond Platnumz.

Huku akizungumzia hayo alikuwa na haya ya kueleza.

 
 

"Nilitumiwa ujumbe katika ukurasa wangu wa instagram na mmoja wa wasimamizi wa WCB, akitaka Collabo,sikuwa na taka hiyo 'story' ijulikane baada ya muda mmoja wa wasanii alinipigia simu na kunikosea heshima

Mimi natambua heshima kuliko pesa katika maisha yangu, ndio wasanii hao huwa wanatoa nyimbo za kupigiwa mfano lakini mimi sina kinyongo na wao

Nilikuwa nataka kikundi chetu kifahamike, lakini si kukosewa heshima." Alieleza Mejja.

Msanii huyo anafahamika sana kwa kuishi maisha ya kawaida, na ambayo si ya kutafuta kiki,

"Kama wewe ni msanii, mtangazaji si lazima uishi maisha fulani ndio watu wafahamu kuwa wafahamika sana

Mimi nakuanga 'mreal' katika maisha yangu, ukiishi maisha ya kawaida hautafanya au kusumbuka katika maisha yako."

Akizungumzia hali ya afya ya mama yake alisema,

 
 

"Mama yangu alikuwa na uvimbe wa kichwa, madaktari hawakuwa wanajua ni nini inamsumbua lakini mwishowe walikuja kugundua kuwa ana uvimbe baada ya kupimwa

Ilifika mahali akapoteza fahamu hakuwa anatujua sisi ni akina nani, lakini sasa anaendelea vyema

Huwa najiita mtoto wa khadija kwa maana mama ndiye alitulea na alipitia mengi."

Kwa mengi zaidi tebelea chaneli ya youtube ya Radiojambo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved