Ukiwa jela lazima uokoke iwapo utakufa uende mbinguni-Julius Wambua

Muhtasari
  • Julius Wambua aeleza jinsi alivyo ishi jela na kuachiliwa huru 
  • Alisema kwamba ni lazima ukiwa jela uokoke iwapo utaaga dunia huende mbinguni

Tunafahamu vyema hadithi yake Julius Wambua ambaye alikuwa amefungwa jela kifungo cha maisha baada ya madai kwamba alimbaka mwanawe wa tatu.

Baada ya ya kumaliza miaka tisa akiwa jela ya Kamiti mwishowe mwanawe alikuja na kubadilisha usemi wake na kusema kwamba hakubakwwa na baba yake ilhali aliambiwa aseme hivyo.

Huku akiwa kwenye mahojiano na radiojambo JUlius alikuwa na haya ya kueleza;

"Nilishikwa mwaka wa 2011 Aprili, nilipokuwa sokoni nikinunua mboga,nilisomewa mashtaka yangu kwamba nimembaka mtoto wangu ambapo alikuwa na miaka 15 wakati huo

mke wangu alinishtaki kwa kosa hilo, nilihukumiwa kifungo cha maisha, nilipokuwa korokoroni hamna mtu ambaye alikuja kunitembelea isipokuwa ndugu yangu na mkewe

ukiwa jela hauna rafiki, rafiki yako ya kipekee ukiwa huki ndani ni Mungu,ukienda hapo kama hujaokoka kwa kweli utaokoka iwapo utakufa utaenda mbinguni." Alieleza Julius.

Huku akieleza nini haswa mtu hupitia jela alikuwa na haya ya kusema.

"Kwa siku ya kwanza ukiingia jela unatamani kujiua kwa ajili ya maisha ambayo unapatana nayo, nilikuwa nimepanga kujiua nilipofungwa lakini nilipatana na mfungwa ambaye tulikuwa tunamuita mwalimu ambaye alinipa ushauri

niliposomewa mashtaka yangu nilihisi heshima yangu imekwisha kwa maana kila mtu alikuwa hapo, nililia machozi ambayo sikuwahi lia tangu nizaliwe

nilifikiria mambo mengi kuhusu mke wangu na mwanangu ambaye alifanya nifungwe maisha,kutoka siku ambayo nilitiwa mbaroni hadi kuenda jela sijawahi zungumza na mke wangu

 

ata angekuja kuniona singekubali lakini nimeshaamsamehe kutoka kwa moyo wangu, unapoingia jela huwa unapewa sare ambayo imeandikwa 'SW' inayomaanisha 'Sahau wazi'sahau kila mtu ambaye unamjua kwa maana hutawahi rudi nje tena."

Julius alizidi na kuelezea jinsi alivyo achiliwa huru;

"Baada ya miaka kadha, niliitwa kwa ofisi na mkubwa lakini nilijificha kwa muda, nilipoenda baada ya kujificha saa moja nilifika kwa mlango na nikamuona mwanangu ambaye alisema nilimbaka

Nilili machozi yakwa kama maji askari akaja kupanguza, mtoto wangu alisema kwamba alikuwa ameambiwa na mama yake na watu wengine aseme kwamba nilimbaka."