Kuna watu ambao hawawezi kufanya kazi na nami kwa maana nilisema mimi ni LGBTQ-Anita Nderu

Muhtasari
  • Anita Nderu hatimaye afungua roho baada ya kuweka wazi kwamba yeye ni jamiii ya LGBTQ
  • Akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba hajali kile watu wanasema kumhusu
  • Pia aliweka wazi kwamba kuna watu ambao wanamuogopa kwa kufunuka kwamba yeye ni jamii ya LGBTQ

Leo studioni tulikuwa naye mtangazaji Anita Nderu a,baye amekuwa akivuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuweka mambo wazi kwamba yeye ni jamii ya LGBTQ.

"Nikiweka kitu kwenye mitandao ya kijamii au nikipakia kitu hayo ni maoni yangu, sijali kuhusu maoni ya mtu mwingine

Ndio kuna wale ambao  wanasema mambo mabaya kunihusu kwenye mitandao na ambao ni marafiki wa karibu, baada ya muda mrefu huwa wananitumia jummbe na kuniomba msamaha mimi huwa nawaambia hukusema hayo hapa nenda kwenye mitandao ya kijamii ukaombe msamaha huko

 

Baada ya kuweka mambo waki kuwa mimi ni LGBTQ, watu walinitoroka na hata wengine kukataa kufanya kazi na mimi kwa ajili ya hayo." Alieleza Anita.

Anita alisema kwamba endapo atapokea simu nyingi kwanza huwa anaenda kuangalia kwenye mitandao ya twitter na kuangalia nini haswa kinatendeka ama iwapo ni yeye anavuma.

Alipoulizwa na Massawe vile mama yake alichukulia ufichuzi wake alikuwa na haya ya kusema.

"Mama yangu hakujua LGBTQ ni nini lakini alinipa mawaidha kwamba nijichunge na nisikasirike, wala kufanya jambo mbaya

Mimi nina mpenzi lakini sipendi sizungumzii sana."