Nilimpeleleza mume wangu lakini hakujua alijua baadaye nilikuwa nimeeka 'tracker' kwa kiatu chake-Jane Mugo

Muhtasari
  • Mpelelezi Jane Mugo aeleza haya kuhusu kazi yake, amedai kwamba hupokea vitisho katika maisha yake lakini amezoea kwa maana ni kazi yake

Tasnia ya upelelezi nchini Kenya imekuwa ikikua kwa kasi. Jane Mugo, mpelelezi binafsi anayedai kusaidia mamia ya kesi, pamoja na hayo kazi hiyo imekua tata kwake.

Leo hii studioni katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye Jane Mugo mpelelezi mkubwa wa kibinafsi Afrika.

Huku akieleza kazi changamoto ambazo amekumbana katika kazi yake alisema kwamba changamoto ni nyingi sana.

 

"Unaweza kuwa umeenda kutatua shida ya familia lakini huwezi enda pekeyako kwa maana hujui utakumbana na nini, nina wafanyakazi kumi katika kampuni yangu nikienda kutatua shida zozote huwa naenda na baadhi ya wafanyakazi wangu

Nilianza kampuni yangu na baiskeli lakini namshukuru Mungu kwa maana saa hizi tumebarikiwa na magari."

KUna wakati Mugo alivuma sana kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari baada ya kudaiwa kuwaalumuua mtu.

Akizungumzia swala hilo alisema,

"Wakati nilipelekwa kortini mwenye alikuwa amenishtaki hakuleta kitu kwa korti, walikuwa wanataka tu kunitishia maisha ili nisiseme ukweli."

Alipoulizwa kuhusu kumpeleleza mumewe kabla ya kifo chake Jane alisema kwamba ashawahi peleleza mume wake bila kujua.

"Ndio nishawahi peleleza Mume wangu, nilikuwa nimeenda nchi za nje lakini hakujua kuwa nampeleleza alijua baadaye

 

Nilikuwa nimeeka 'tracker' kwa kiatu chake, nilimpata kwa nyumba ya mwanamke, mume wangu aliaga dunia miaka 15 iliyopita

Mimi sijawahi kosa mwanamume kwa ajili ya kazi yangu." Aliongea Jane.

Jane alisema kwamba ametishiwa maisha mara nyingi kwa ajili ya kazi yake, lakini amezoe kwa maana hiyo ngio kazi yake.