Mizimu ya uganga na uchawi ilifanya niachie masomo yangu darasa la 5-Apostle Martin Mulu

Muhtasari
  • Apostle Martun Mulu aeleza jinsi alikuwa mganga akiwa na miaka 2, huku mwishowe akiokoka na kuwa mtumishi wa Mungu

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Apostle Martin Mulu, ambaye kabla ya kuwa mtumishi  alikuwa mganga na mchawi.

Huku akieleza safari yake ya kuokoka na jinsi aliacha shule kwa ajili ya uganga alikuwa na haya ya kusema.

"Baba yangu alikuwa na bibi 17 akawapa talaka 12 na akabakisha 5 miongoni alikuwa mama yangu, niliambiwa kwamba nilipozaliwa tu hivyo baba yangu na watu wengine walianza kusema kwaba mimi ni mchawi kwa maana baba yangu alikuwa mganga hatari kitui

 

Nilisoma hadi darasa la tano lakini mizimu ikakataa nisome nikaanza kuota ndoto za misimu ya uganga na uchawi, mwaka wa 1988 nilikuja Nairobi nikaanza kutibu watu

Wateja wangu wengi walikuwa wanawake." Alieleza Martin.

Pia Martin alifichua kuwa alikuwa anashika nyota za watu ili wasiendelee lakini ilifika mahali nikasema niokoke.

" Nlianza kuona ndoto za uganga na uchawi nikiwa na miaa miwili Zile mali nilikuwa nazo nikiwa kwa uganga hazikunisaidia ndio maana nimeokoka ili nisaidike."

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo youtube.