Lengo langu kuu ni kumpiga Khaligraph Jones-Hatimaye Eric Omondi afichua haya

Muhtasari
  • Mchekeshaji Eric Omondi afichua haya kuhusu maisha yake, huku akisema lengo lake kuu ni kumpiga Khaligraph jones
  • Pia alisema kuwa kipindi cha Wife material kinarejea hivi karibuni

Kwa kweli nani hamfahamu na kumjua mchekeshaji Eric Omondi kwa mambo ambayo amekuwa akifanya, aya basi hii leo studioni tulikuwa naye mchekeshaji huyo ambeye alifichua mambo kadha wa kadha.

Alipoulizwa na Massawe Japanni lengo lake kuu ni lipi alisema kwamba lengo lake ni kumpiga Khaligraph Jones tarehe 23 Februari.

"Lengo langu kuu ni kumpiga Jones, siendi zoezi kwa ajili ya afya yangu lakini kwa ajili ya kumpiga Jones

 

Nilihudhika wakati Khaligraph, aliponiiunua kama mtoto mbele ya mashabiki wangu na wake baada ya kuwa msamaria mwema

ni jambo amalo lillinisumbua sana,najua watu wengi wananidharau lakini katika vita vyangu na Khaligraph ni kama Daudi na Goliath, mimi nitakuwa na Mungu na yeye na nguvu yake," Alisema Eric.

Pia alifichua kuwa kipindi cha Wife material season 2 kinakuja ambapo atatafuta mke wake.

"Nataka wanawake 5 wakenya,5 wa uganda na 5 watanzania, mwaka huu nitakuwa na harusi, kati ya kipindi hicho hapo ndipo nitaoa kwa yule atashinda, pia wanapaswa kuwa na miak 23 na kupanda

hivi karibuni nafikisha miaka 40 na nataka kuwa na familia yangu,"

Kwa hakika kila mtu ana majuto katika maisha ya lakini Eric aliweka wazi kwamba hana majuto katika maisha yake.

PIa alisema kwamba anatamani wazazi wake wangekuwa hai waone kazi ambayo anafanya.