(+Video)Nililia mwaka wa 2007, baada ya baba yangu kushindwa katika uchaguzi mkuu-Winnie Odinga

Muhtasari
  • Winnie Odinga asema alilia mwaka wa 2007 baada ya baba yake kuoteza uchaguzi mkuu
  • Pia alisema miaka hiyo nyingine ambayo baba yake amekuwa akipoteza uchaguzi mkuu hajalia
  • Winnie alisema sisasa iko katika damu,na kuwa ni jambo la furaha sana kufanya kazi na baba yake

KInara wa chama cha ODM Raila Amollo Odinga amewania kiti cha urais mara nne bila ya kufaulu.

Mwanawe Winnie Odinga akiwa kwenye mahojiano na radiojambo aliweka wazi kwamba kuna wakati walilia kama familia baada ya baba yake kupoteza uchaguzi huo.

"Mwaka wa 2007 wakati wa uchaguzi mkuu, wakati baba yangu alipotezza uchaguzi mkuu wa urasi, 2007 ni lilia

 

Mwaka wa 2017, baada ya Raila kupoteza uchaguzi mkuu, aliapishwa katika bustani ya Uhuru wakati huo kila mtu mwenye alikuwa katika hafla hiyo alikuwa ameweka maisha yake hatarini

Nilimsaidia baba yangu kama vile huwa nasaidia familia yangu na wala si siasa, siasa iko kwa damu yangu," Alieleza Winnie.

Wakati wa hafla hiyo Winnie alifichua kwamba babayake, Raila hakutaka ahudhurie hafla hiyo bali alimwambia lazima awe naye.

"Baba yabgu hakutaka niende katika hafla hiyo, unakumbuka vile aliyekuwa rais wa marekani Kennedy vile alipigwa risasi na mke wake akamshika, niliambia baba yangu kuwa nitakuwa hapo kitendo hicho kikitokea,"

Winnie aliweka wazi kwamba ni jambo la kupendeza kufanya kazi na baba yake.

Hii hapa video ya mahojiano hayo;

Radio Jambo Kenya | Ongea Usikike | Ni kituo nambari moja Kenya kwa matangazo ya kiswahili. Vipindi vyake vina jumuisha Spoti,Mijadala moto moto na muziki wa Kiafrika #RadioJamboKenya Subscribe to RadioJambo Youtube - https://bit.ly/39wwc6u Mitandao ya Kijamii Instagram - https://rb.gy/e154d1 Facebook - https://rb.gy/09d1b9 Twitter - https://rb.gy/e23220