Kuwa mzazi kumenibadili sana katika maisha yangu-Muigizaji Nick Mutuma

Muhtasari
  • Nick Mutuma aeleza jinsi kuwa mzazi kumebadili maisha yake huku akisema kwamba kulea ni kazi ngumu
Nick Mutuma

Leo katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye muigizaji Nick Mutuma ambaye alifunguka kuhusu maisha yake.

"Nilianza kazi ya uigizaji mwaka wa 2008, ambapo niliigiza kama mwanamume mbaye anapenda 'sugarmummies' wazazi wangu walishangaa sana lakini niliwaeleza

Nimekuwa na Bridget Shighadi kwa miaka kumi, kuna wakati nilimezea mwanamke mwingine mate lakini ni kawaida ya wanaume kusifu urembo wa mwanamke mwingine," Alisema Mutuma.

 

Alipoulizwa kwanini mara kwa mara huwa hawapakii picha zao pamoja Nick alikuwa na haya ya kusema.

"Tunapenda maisha yetu yawe ya siri kando na uigizaji, Bridget si mwanamke ambaye anapenda kiki wala kuweka maisha yake hadharani

kuwa mzazi kumenibadilisha sana, kwa maana nimeacha kuzurura kila mara, kulea si jambo rahisi kwa hakika

Mahali tumefika kama wapenzi wawili katika sekta ya uigizaji kuna uigizaji mwingine hatuwezi fanya,"