Mtoto wangu alikuwa ananiosha baada mimi kukeketwa-Mwanamke asimulia kwa machozi

Muhtasari
  • Mwanamke aeleza aliyopitia baada ya kukeketwa, huku mumewe akienda mafichoni
  • Nyambura alisema kwamba mama yake aliaga dunia baada ya kumzaa huku akilelewa na baba yake pekee

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Nyambura ambaye alisimulia hadithi yake alipokuwa mtoto na hata katika ndoa.

Nyambura alisema kwamba mama yake aliaga dunia baada ya kumzaa huku akilelewa na baba yake pekee.

"Mama yangu aliaga dunia baada ya kunizaa, nikiwa darasa la nane muhula wa kwanza baba yangu aliaga dunia na kuanza kupata shida

 

Kuna mwanamume ambaye alikuwa ananiita na naosha vyombo kisha ananipa chakula, nikiosha vyombo nilikuwa natoa ukoko wa ugali nakula na kisha nampelekea dada yangu chakula kwa maana alikuwa mjamzito

Huyo mwanamume alinioa nikiwa na miaka 14,alinipata nikiwa malkia, nilijifungua watoto wawili kisha akaanza kutoka nje ya ndoa

Nikimuuliza alikuwa ananipa visababu vyake na kunichapa kichapo cha mbwa," Alieleza Nyambura.

Enzi zile wnawake walikuwa lazima wakeketwe, kisa ambacho kilifanya ateseke kwa miaka huku mwanawe kifunguoa mimba akiwa na miaka mitatu akimtunza na hata kumuosha.

"Mtoto wangu wa pili aligonjeka sana nikalazwa miezi miwili katika hospitali kuu ya Kenyatta, baada ya kutoka siku chache zilipita

Nilienda kutafuta kibarua nifanye, nilipatana na kikundi cha akina mama, walinivua nguo na kuanza kunichapa, hawakunipa sababu yao ya kinichapa nikiwa uchi 

Licha ya yangu kuomba msamaha hawakuacha kunichapa,siku moja walikuja kwangu kwa nyumba wakanivua nguo na kuanza kunichapa tena

 

Mmoja wao aliniulizwa kama nimekeketwa, walitoa wembe na wakanikeketa papo kwa hapo,mama mmoja alsema kwamba niwekwe alama ili kuonyesha nimekeketwa

Nilikatwakatwa na wembe huo kwenye mapaja yangu, hadi leo nina alama za kukatwa, baada ya kunikeketa waliniweka tumbaku ambayo ilikuwa inaniwasha sana,"

Nyambura alizidi kusimulia hadithi yake,

"Baada ya siku walinichukua na kuenda kunifungia mahali na kisha watoto wangu wakachukuliwa, wakati huo mume wangu alikuwa amejificha,nilipotoka hapo nilienda nyumbani mtoto wangu alikuwa na miaka 3 ambapo alinitunza wakati huo ata kunipeleka msalani

Amepitia sana,alikuwa ananifulia nguo zangu za ndani baada ya kuendea haja ndogo kama sijui lakini alikuwa anajua

Baada ya kupona mume wangu alirejea na kufanya ngono na mimi mbele ya watoto wake, nilipokataa aliniambia wacha watoto wake waone mahali walitoka

Amekuwa akinitishia maisha, nilienda kuripoti kwenye kituo cha polisi lakini sijawahi pata haki, mtoto wangu ambaye alikuwa ananitunza baada ya kukeketwa sasa yuko darasa la saba,"

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo youtube.