Nilipopakia video nikiwakaribisha kanisani sikuwa najaribu kuonyesha umbo la mwili wangu-Nicah the Queen

Muhtasari
  • Msanii Nicah the Queen aweka mambo haya wazi, baada ya kuachana na Ofweneke
  • Pia alisema kwamba hakuwa anajaribu kuonyesha umbo la mwili wake alipopakia video akiwakaribisha mashabiki kanisani
Nicah the Queen
Image: Studio

Studioni tulikuwa naye msanii Nicah the Queen na ambaye ni mama wa moto wake mchekeshaji DROfweneke.

Huku akizungumzia uhusiano wake na Ofweneke na bibiye Ofweneke alikuwa na haya ya kusema,

"Uhusiano wetu haukuwezekana, lakini Ofweneke ni baba mzuri naamini Ofweneke sana, mimi na mkewe hatujaongea lakini watoto wangu huniambia kwamba ni mzuri

 

Pia ni mrembo, na ni mama mzuri," Nicah Aliongea.

Alipoulizwa anachukulia vipi jinsi wanamitandao walimlinganisha na mkewe Ofweneke  alikuwa na haya ya kusema,

"Mashabiki wetu huwa tunawahitaji, wakisema chochote niko sawa, lakini kunilanganisha na mkewe Ofweneke hamna shida kwa maana kila mtu ana maisha yake

Sijaacha muziki lakini nilipoachana na baba wa watoto wangu, nilikuwa napitia mengi lakini mwaka huu nitarejea,"

Mapema wiki hii Nicah alikejeliwa sana kwa kupakia video huku akiwakaribisha mashabiki kwenye mitandao,

"Sikuwa na ubaya wala sikuwa najaribu kuonyesha umbo la mwili wangu, ukweli dada yangu ndiye alichukua video hiyo lakini hakuwa achukue nyuma yote

Lakini licha ya yote lazima niwaalike kanisani, nani alisema unapaswa kuvalia nguo fulani kanisani,"