Niambiwe ukweli kilichosababisha kifo cha mtoto wangu hadi leo sijaambiwa-Mama Jeniffer asema

Muhtasari
  • Mama yake Jennifer asimulia hajui sababu ya kifo cha mwanawe

Binti mmoja wa miaka nane alianguka na kufariki aliposimama kujibu swali la hesabu katika shule ya msingi ya New View iliyo Kayole.

Waalimu walisema kuwa Jeniffer Ouma ambaye alikuwa katika daraja la pili alianguka alipokuwa anajibu swali siku ya jumatano wiki iliyopita.

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye mama Jeniffer ambaye alieleza kinagaubaga jinsi mwanawe alipotea na kumpata akiwa hospitalini.

Hilda Achieng alisimulia na kusema kwamba hajafahamishwa nini kilisababisha kifo cha mwanawe hata baada ya upasuaji wa mwili kufanyika.

"Mtoto wangu hakuwa mgonjwa alikuwa mwenye afya nikimpeleka shuleni, daktari aliniambiwa kwamba mtoto wangu alipelekwa hospitalini na watu wanne

Nilipompata mtoto tulianza uchunguzi, lakini polisi wa DCI kutoka Kayole aliniambia niache afanye kazi yake, hawataki niongee,mwalimu wa darasa la mttoto wangu, na mwalimu mkuu sijazungumza na wao

Nilimuona mwalimu mkuu siku ya upasuaji wa mwili wa mtoto wangu, lakini hakuzungumza na mimi, alikuwa anazungumza tu afisa wa polisi ambaye anafanya uchunguzi

Sijawahi letewa ripoti ya upasuaji, na kufahamishwa nini kilisababisha kifo cha mtoto wangu, nataka kuambiwa nini kilisababisha kifo chake tu, kwa maana sijawahi ambiwa wala kufahamishwa

Polisi huyo hataki niulize walimu wa shule maswali, mwili wa mtoto huko kwenye makafani, lakini sijui gharama nitalipa na nini," Alieleza Hilda.

Kulingana na Hilda marafiki  wa mwanamwe walisema kwamba mwalimu alimchapa mwanawe nyuma ya kichwa na wakapewa shilingi 30 ili wasiseme chochote.

"Naomba Kinoti na Matiang'i waingililie kati kesi yangu, kwa maana watoto walishuhudia kile kilitendeka na mtoto wangu,"