Mpango wa kando wa mume wangu aliniambia pia nami nitampata mwanamume ananipenda-Rose Williams asema

Muhtasari
  • Rose aeleza jinsi alimpikia mpango wa kando wa mumewe bila ya kujua
Rose Williams
Image: Studio

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye Rose Williams ambaye alimkaribisha mpango wa kando wa mumewe bila ya kujua kwamba ni mpango wake.

Kulingana na Rose alimpikia mpango wa mumewe, kwa madai kwamba amekuja kutembelea mtoto wao kwani alikuwa mfanyakazi wao.

"Mume wangu alianza kubadilika, akaanza kubeba vitu yake moja kwa moja, baada ya mtoto wangu kufikisha miaka 4 alibeba kila kitu na akaenda

Baada yangu kujifungua mtoto wangu alikuwa na mwezi mmoja, mpango wa kando wa mume wangu alikuja kunitembelea na na nikampikia

Sikujua kwamba ni mpango wake, nilipogundua nilimpigia simu nikamuuliza kwanini alifanya hayo ilhali nilikuwa namtunza vyema kama wafanyakazi wengine 

Aliniambia kuwa nami nitampata mwanamume ambaye ananipenda kama vile mume wangu anampenda, ni miaka 4 sasa tangu tutengane," Alieleza Rose.

Rose pia alimshukuru Mungu kama hakuokota makaratasi, kama mwendawazimu.

"Nashukuru Mungu si kuokota makaratasi kwa barabara, kwa maana nilikuwa naumwa sana moyoni, kwanza nikimpigia simu alikuwa anampa mwanamke huyo nizungumze naye

Kwa sasa sina mchumba nataka nichukue muda wangu tu, walifanikiwa na mtoto mmoja na popote mahali walipo nawatakia mazuri maishani mwao

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.