Safari yangu ya kufanya kazi na BBC ilikuwa imefika mwisho-Makena

Muhtasari
  • Makena azungumzia safari yake ya BBC
Makena Njeri
Image: Studio

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Makena Njeri ambaye hapo awali alivuma sana mitandaoni baada ya kujitokeza na kusema kwamba yeye ni shoga.

Huku akizungumzia suala hilo aliuwa na haya ya kusema;

"Ukweli wangu ulianza kutangazwa na watu kabla yangu kuusema, nilifikiria kwamba Mungu ametupa uwezo wa kusema ukweli, hapo ndipo niliamua kujitokeza na kusema ukweli wangu

Hii ni safari ya kujikubali,jambo ambalo watu wengi wako nalo ni kupuuza ukweli na hawajahelimishwa

Sikujitambulisha kwa ajili yangu bali kwa kila mtu ambaye anapitia jambo kama langu,fanya jambo kwa ajili ya jamii," Alisema Makena.

Makena pia akizungumzia safari yake ya kutoka katika kampuni ya BBC alisema kwamba safari yake ilikuwa imefika mwisho kwani ni jambo ambalo alifikiria kwa muda mrefu.

"Nilifanya kazi katika kampuni ya BBC kwa miaka 3,safari yangu ya kufanya kazi ilikuwa imefika mwisho, kwani sio jambo la kuamka na kusema kwamba unataka kutoka

Ni matamanio ya kila mwanahabari kuendikwa na kampui ya BBC, hatua yangu ya kutoka katika kampuni hiyo nilikuwa nimefikira kwa zaidi ya mwaka mmoja,"

Makena alisema kwamba ana maazimio ya kuwa na familia.

Kwa mengi zaidi tembelea radiojambo youtube.