Raila ndiye sababu yangu ya kufahamika namshukuru-Shebesh

Muhtasari
  • Shebesh aweka wazi kwamba Raila ndiye alifanya afahamike kwenye sekta ya siasa
Rachel Shebesh na Massawe Japanni
Image: Studio

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Katibu mwandamizi wa huduma kwa umma Rachel Shebesh ambaye alihitimu miaka 50 wikendi iliyopita.

Huku akizungumzia safari yake ya siasa Shebesh aliweka wazi kuwa anamshukuru Raila kwa maana ndiye alifanya afahamike haswa katika sekta ya kisiasa.

"Raila Odinga ndiye sababu yangu ya kufahamika sana katika siasa, kama sio yeye singekuwa mahali nilipo na namshukuru sana

Nataka kuwashauri wanasiasa ambao wanatoka katika vyama vya siasa wanapaswa kutoka kwa heshima, nilipotoka katika chama cha ODM nilitoka na heshima,"

Pia mwanasiasa huyo alikuwa mwakilishi wa wanawake wa kwanza katika kaunti ya Nairobi, na akizungumzia kazi yake ambayo huwa anajivunia nayo alipokuwa kwenye usukani alikuwa na haya ya kusema.

"KIle kitu najivunia ni vile niliweza kuwasaidia watu walemavu na watoto walemavu,na wakati Esher Passaris alishinda mwaka wa 2017, nilimwambia aendeleze kazi ambayo nilikuwa nimeanzisha na ameweza kufanya hayo

Siwezi kumlaumu mtu yeyote kwa kupoteza, kiti mwaka wa 2017,sianamengi ya kujihusisha nayo katika uchaguzi mkuu ujao nataka tu kuwatumikia wananchi,"Shebesh alizungumza.