Sijawahi muona baba yangu,nilimuona siku ya mazishi yake-Rich Mavoko afichua

Muhtasari
  • Rich Mavoko afichua haya kuhusu maisha yake ya utotoni
Msanii Rich Movoko
Image: Studio

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye msanii kutoka Tanzania Rich Mavoko. ambaye amekuja Kenya kuzindua albamu yake.

Kuna kipindi ambacho Mavoko alikuwa, kwenye lebo ya muziki ya Wasafi, msanii huyo aliweka wazi kuwa kabla ya kujiunga na WCB alikuwa anaimba.

"Nilikuwa ninaimba kabla ya Wasafi. Mimi sikutafuta Wasafi. Nilianza kuimba baada ya kumaliza kidato cha 4. Nina watoto 2, mama tofauti waliniachia watoto na wao wakaendelea na maisha yao

Mimi ni mtoto wa 5, kitinda minda. Sisi tumelelewa na mama tu. Sijawahi kumuona babangu ila tulikuwa tunazungumza. nilimuona siku ya mazishi yake," Aliongea Mavoko.

Huku akizungumzia usanii wake msnii huyo alisema,

"Nina maono makubwa sana na maono yangu yanategemea support ya mashabiki wangu. Nitatoa albamu yangu mwaka huu.."