Mume wangu alimuoa mwanamke mwingine na pesa nilizokuwa namtumia nikiwa Saudi Arabia-Faith

Muhtasari
  • Faith asimulia mateso aliyopitia akiwa Saudi Arabia
  • Mume wangu alimuoa mwanamke mwingine na pesa nilizokuwa namtumia nikiwa Saudi Arabia-Faith
Image: Studio

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye Faith, ambaye alisimulia mateso ambayo alipitia akiwa Saudi Arabia.

Kulingana na Faith sio waajiri wote ambao ni wabaya, lakini yeye alipatana na waajiri ambaye walikuwa kama shetani, yaani hawakuwa na roho ya utu.

Faith amesema kwamba alipokea mateso kwa mwaka mmoja na miezi mitano, licha ya kutaka usaidizi lakini nguvu zake zinaambulia patupu.

"Nilifanya kazi Saudi Arabia kwa mwaka mmoja na miezi mitano, nilipatana na waajiri amao hawakuwa wazuri, lakini sio wote ambao ni wabaya 

Mwajiri mwanamume, ndiye alikuwa mbaya zaidi katika mwezi wangu wa sita, niliuwa nataka usaidizi ili nitoke maeneo hayo, mwanamume huyo alipojua kwamba natafuta usaidizi, alinichapa mpaka akaniumiza ilhali mke wake hakunitetea

Kuna wakati nilikuwa jikoni nikipika, nilikuwa naskia nimeisha nguvu, mwanamume huyo alichukua maji ambayo nilikuwa nayachemsha kupinduka alinichoma mkono

Alichukua bunduki na kuekelea kwa meza na kuniambia kwamba, niseme nilijichoma, kwa maana nikisema alinichoma atanipiga risasi ni kufe

Nilirekodi video na kusema yale alikuwa ameniamba ni seme, hakunipeleka hospitali baada a hayo nilitoroka na kuenda hospitali," Alizungumza Faith.

Baada ya kuwasili nchini jambo ambalo lilimshangaza ni maisha ambayo mume wake walikuwa anisha lich ya kumtumia mshahara wake wote.

"Nilipowasili nchini mume wangu alinikujia kwenye uwanja wa ndege, alinipeleka kwa nyumba ambayo ilikuwa tu na gondoro pekeyake na kuniambia amekuwa akiishi hayo maisha

NIlipowauliza majirani waliniambia kwamba alihamia hapo wiki mbili zilizo pita,kumbe pesa ambazo nilikuwa namtumia alizitumia kuoa mwanamke mwingine,"

Kwa mengi zaidi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.