'Nilifukuzwa na mama wa kambo nikiwa na miaka 16-Msanii B Classic afunguka kuhusu maisha yake

Muhtasari
  • Msanii B Classic afunguka kuhusu maisha yake
Msanii B Classic
Image: Studio

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye msanii Denis maarufu B Classic, ambaye alisimulia maisha yake ya utotoni.

B Classic alivuma sana baada ya kumpa  au kumnunulia mchekeshaji Omosh kamera na Tripod.

KUlingana na msanii huyo kutoka kaunti ya Taita Taveta mama yake alimuacha akiwa na miaka 3 huku akilelewa na mama wa kambo.

"Baba yangu na mama yangu walitengana, lakini mama aliniacha mikononi mwa baba yangu, ambaye alioa mama wa kambo

Baada ya kuhitimu miaka 16 mama wa kambo alinifukuza nyumbani, nilianza kazi ya kulisha ng'ombe kwa miezi kumi lakini mama huyo hakunilipa chochote

Sasa hivi ninachumbia muziki. Hizi barabara ni mbaya sana. Nimekuja Nairobi 2018 kutafuta wafadhili wa muziki wangu

Niliona mataa Mlolongo, nikashuka gari nikifikiri nimefika Nairobi. Nilikuwa nimetoka kijijini.

Nilipoteza matumaini kwa muziki 2019 nikarudi kijijini maanake nilikuwa ninafanya muziki lakini hunisaidii," Alisimulia B Classic.

Pia alisema kwamba mama yake alifukuzwa kwa ajili ya mzozo wa kifamilia, na kumueleza kwa nini alimuacha.

"Nampenda mama yangu sana kwani alinieleza kwanini aliniacha, mama wa kambo nilimsamehe na tunaendelea na maisha."

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.