Watu wa familia walichukua mali yetu baada ya wazazi wangu kuaga dunia- Muunda maudhui Shorn Arwa

Muhtasari
  • Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye munda maudhui Shorn Arwa ambaye alifahaika sana mwaka jana baada ya kuigiza, mchezo unaouhusiana na kisasi cha sasa haswa wanawake
  • Muunda maudhui Shorn Arwa afichua mali yao ilichukuliwa baada ya wazazi wake kuaga dunia
Shorn Arwa
Image: Studio

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye munda maudhui Shorn Arwa ambaye alifahaika sana mwaka jana baada ya kuigiza, mchezo unaouhusiana na kisasi cha sasa haswa wanawake.

Shorn amekuwa akiigiza na wasanii tofauti miongoni mwao ni mcheshi Mammito, ambaye anafahamika sana kupitia uchekeshaji wake.

Huku akizungumzia uigizaji wake kuhusu 'wababa' amesema kwamba watu wengi wamekuwa wakimuita kwa jina hilo, kwani baadhi yao hawajaelewa kuwa ilikuwa tu uigizaji.

"Mimi ni mtoto wa 5 katika familia ya watoto 6... Kila mtu huniita yule dame wa wababa. Yule mtu anaamini kwamba maisha ya mitandaoni ya kijamii ni ya uhalisia basi ana mchezo... Nimechumbia mwanaume wenye umri mkubwa kuniliko (wababa) ... 

Ningehisi vibaya kitambo ila sasa nimezoea maanake nimekuja kugundua kuwa ni kuwahusu na si kunihusu... Ninafikiri mimi ni mtu wa kawaida aliyeona fursa na akaitilia maanani. Nimesomea saikolojia... Nilijigundua mwenyewe..." Shorn Arwa alizungumza.

Pia alisema kwamba amechumbia watu ambao wamemshinda umri na miaka 5 ila anapata yeye ndiye anaongoza hayo mahusiano.

"Nimechumbia pia watu ambao wamenishinda kwa miaka kama 5 ila ninapata kwamba mimi ndio ninaongoza hayo mahusiano. Ninahisi kwamba hawa vijana wanakuwa kama watoto wangu. Nimekuzwa na dadangu. Mamangu aliaga dunia nikiwa na miaka 6 na baba nikiwa na 7..." Shorn Arwa.

Kulingana na Shorn baada ya wazazi wake kuaga dunia jamaa zake walichukua mali yao na kuwaacha bila chochote.

"Wakati wazazi wangu waliaga dunia, watu wa familia yetu walichukua mashamba, manyumba, kila kitu. Dadangu akatulea. Naye alikuwa mwerevu, alipata ufadhili kusoma

Mama yangu aliaga nikiwa na miaka 6 na kisha baba yangu akaaga nikiwa na miaka 7."

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.