Hatujaachana na mkewe wangu-Msanii KenRazy afunguka

Muhtasari
  • Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye msanii KenRazy, ambaye awali uvui ulienea kuwa ameachana na mke wake Sosuun
KenRazy
Image: INSTAGRAM/KenRazy

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye msanii KenRazy, ambaye awali uvui ulienea kuwa ameachana na mke wake Sosuun.

Akiwa kwenye mahojiano hayo, msanii huyo alifunguka na kuweka wazi kwamba wawili hao wako pamoja.

"Mimi ni mke wangu tuko pamoja, na wala hatukuachana, shida ilitokea ambapo  kulikuwa na mzozo kwenye familia

Lakini kama mwanamume nilitatua tatizo hilo, la mke wangu na dada zangu, nilichojifunza ni kuwa kama mwanamume wa nyumba unapaswa kutatua shida kama mwanamume

Pia hupaswi kumuonyesha mke wako kwamba unapenda sana familia yako kumliko,au kuonyesha familia yako unampenda mke wako kuwaliko," Alizungumza KenRazy.

HUku akizungumzia kwa nini amekuwa kimya kwenye sekta ya usanii msanii huyo alikuwa na haya ya kusema.

"Baada ya bendi ya Grand Pa kuvunjika, singeweza kuanza kutoa kibao kwa haraka, kwani nilijua kulikuwa na mzalishaji na meneja, albamu yangu ambayo nimetoa kwa sasa nilikuwa niitoe mapema lakini corona ikaingia nchini

KIle naweza waambia mashabiki wanu kuwa sitanyamza tena sana, lakini wanishike mkono na kusikiza albamu yangu ya 'Son of God'."

KenRazy amebarikiwa na wasicha wawili wenye umri wa miaka 10 na 3.

Pia aliweka wazi kwamba anampenda mke wake,na kumshukuru kwa kuwa naye kwenye safari yake ya muziki.