Mama yangu ni kama dada yangu,Brenda Jons hajawahi kuwa rafiki yangu-Phoina afichua haya

Muhtasari
  • Phoina afichua haya huku akikana kuwa rafikiye Brenda Jons
Phoina
Image: Radiojambo

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Phoina, ambaye alifichua mambo kadha wa kadha katika maisha yake.

Kulingana na Phoina mama yake amekuwa akimsaidia sana katika biashara yake na hata maishani mwake.

Phoina pia amesema kwamba katika chuo kikuu alikuwa amesomea shahda ya uanahabari, ilhali akabadilisha kazi yake na kuanzisha baishara ya vipodozi.

"Siku zote nilitamani kuwa na ndugu lakini sikukosa chochote, mama yangu alikuwa na miaka 19 nilipozaliwa, ni kama dada kwangu, niko naye kila wakati, ndiye msaidizi wangu nambari moja. baraka kwa ajili yangu. Sikupeza kuwa na ndugu."

Phoina hivi majuzi alizindua duka lake la vipodozi katika Barabara ya Riara ambako anauza bidhaa mbalimbali za urembo.

"Ni katika barabara ya Riara, kituo cha Sebuleni. Nimekuwa nikipenda vipodozi tangu nikiwa mdogo. Mama yangu alikuwa akipenda urembo. Kuna wakati nilifukuzwa shuleni kwa kuwapodoa wanafunzi wengine," alisema.

"Nilikuwa nikitengeneza nywele za mama yangu na bibi yangu. Nilifanya utangazaji na nilitaka kuwa mtangazaji wa TV. Baada ya mafunzo, sikutaka kufanya hivi. Ilikuwa ngumu kwangu. Kuzungumza hewani ilikuwa msongo wa mawazo. Ninaamua kufanya kitu ambacho nilipenda."

Pia akiwa kwenye mahojiano alikana kuwa rafiki yake Brenda Jons.

Waili hao walivuma mitandaoni mwaka jana baada ya Brenda kudai kwamba Phoina alimnyang'anya rafiki yake, jambo amblo Phoina amekana.

"Hajawahi nipigia simu na kuniuliza kuhusu jambo hilo, simkani lakini Brenda hajwahi kuwa rafiki yangu, kama ana shida nami aje moja kwa moja kwangu."

Aidha amesema kwamba hana mchumba kwani anazingatia biashara yake na wakati atakapo kuwa tayari atazingatia kuwa na mpenzi.