Watoto wangu 2 ni wasanii-Mercy Masika afichua

Mercy amewasihi mashabiki wake kumpa Mungu muda wao kila siku.

Muhtasari
  • Nafikiri kuna njia inayofaa na njema zaidi ambayo Eric angetumia kuzungumzia suala la wasanii wa nyimbo za injili
Msanii wa injili, Mercy Masika
Msanii wa injili, Mercy Masika
Image: instagram/mm

Katika kitengo cha ilikuaje na mtangazaji Massawe, tulikuwa naye msanii wa nyimbo za injili Mercy Masika.

Huku akizungumzia matamshi ya Eric Omondi ambapo alisema kwamba wasanii wanaishi maisha ya uongo Mercy alisema;

"Hali ambayo tuko kama wasanii wa injili inaonyesha hali ambayo kanisa liko na kama nchi Nzima, tuko kwenye kitanda cha hali mahututi tunahitaji kuamka,tumekuwa na shida kama wasanii 

Nafikiri kuna njia inayofaa na njema zaidi ambayo Eric angetumia kuzungumzia suala la wasanii wa nyimbo za injili

“Tasnia ya injili inaonesha picha halisi ambayo mtu yeyote anapitia, kuna kupanda na kushuka. Inawezekana ndio kuna kulegea mahali lakini hilo halimaanishi kwamba injili inafifia, nahisi kuna ukombozi mkubwa wakati huu kuliko wakati mwingine wowote

Vyombo vya habari vimekuwa vikiandika  maneno hasi kuhusu injili, na kuacha upande ule mzuri kwa miaka 3 sasa,"Mercy amesema.

Mercy alisema kwamba ametembea kwenye mataifa mengi na ameona watu wakiishi katika hali duni kuliko Kenya.

Alisema kwa njia nyingi Wakenya wamebarikiwa lakini hawaoni, kisa kulalamika kwa kila kitu, huku pia akisema nguvu nyingi hutumika katika kuangazia masuala hasi katika jamii.

"Nimebarikiwa nikatembea sana Afrika. Kenya tumebarikiwa sana lakini hatujui. Ukitembea sana Afrika utajua kwamba tumebarikiwa. Barabara, afya, amani. Huwa tunalalamika sana. Tasni ya injili haijafa, haifi... Watoto wetu wawili wanaimba, hatuwalazimishi. Tumerekodi nyimbo zao. Hivi karibuni tutakuja kupiga kelele..."

Msanii huyo amezungumzia idadi ya manabii ambayo imeongezeka na kusema kwamba manabii ni wengi na kila mtu ana mafunzo yake.

Mercy amewasihi mashabiki wake kumpa Mungu muda wao kila siku.