Mama ya mbunifu wa mapambo Jeff Mwathi asema kuwa hataki na hawezi kuzungumza na mshukiwa wa mauaji ya mwanawe, Dj Fatxo.Siwezi kuzungumza na mhusika mkuu wa mauaji ya mwanangu!- Mamamke Jeff
Hannah Wacuka, akizungumza kwa njia ya kipekee katika kipindi cha Radio Jambo, alimuambia Massawe Jappani kuwa hawezi kuzungumza na mtu ambaye anashuku kuwa mhusika mkuu kwa kifo cha mwanawe.
Mama huyo akizungumza na huzuni tele alisistiza kuwa Faxto alihusika katika mauaji hayo baada ya kumwalika mwanawe katika nyumba yake siku hiyo ya mauaji.
"Hio ilikua mpango wa huyo Dj, alimuita kijana wangu kwa nyumba yake na nina ushahidi wa video kwa simu yangu ya hawa wawili walishinda pamoja siku hiyo" Hannah alisema.
Alipoulizwa kama amewai kuzungumza na Dj huyo, Hannah aliyejawa ghahabu alisema kuwa hawezi kuzungumza na mtu ambaye anashuku alihusika kwa kifo cha mwanawe.
"Siezi zungumza na huyo dj mimi sina kitu ya kuzungumza na yeye," Aliongeza Hannah.
Aidha aliongeza kuwa anahisi kuwa serikali ilikua inatia kila juhudi kuhakikisha kuwa keshi hio inafunikiwa na kusahaulika.
"Polisi imtafute aseme kwa nini alimuua na alimuua aje. Serikali inafaa kuchukua hatua, wanasema ati vyombo vya habari ndio iliiingililia na si hvyo, mtoto wangu aishi kuwasumbua ata na kwa kizazi chao," aliosema kwa uchungu.
Wiki jana baada ya Fatxo kupitia kwa mawakili wake kuiandikia DPP kuhusu kutaka majibu ya uchunguzi wa mauaji ya Jeff, DPP walitoa ripoti hiyo na kumtolea mashtaka yote.
Fatxo alisema alikuwa amechafuliwa jina kwa kiasi kikubwa na kuwasihi wafuasi wake kumuunga mkuno ili kulisafisha jina lake.