Amekuwa akinipiga siku mingi, si mara ya kwanza-Mtumba Man azungumzia kupigwa na mkewe

Amedai kuwa, wakati mmoja mpenziwe aliwahi kumchoma na kisu alipomuuliza kuhusu vitendo vyake.

Muhtasari

•Mtumba man alisema kwamba malumbano kati yake na mpenzi wake yamekuwa yakiendelea kwa muda mpaka pale alipoamua kuweka wazi kwa umma.

•"Sijawahi kupiga mwanamke, na kila mara akianza vita, huwa namshika tu ili kuzuia vita kuendelea kwani sikuwahi taka kumuumiza." alisema.

Sande Mayua,Mtumba Man
Mutuba man Sande Mayua,Mtumba Man
Image: Hisani

Mtayarishaji maudhuhi Sande Mayua,anayetambulika kwa jina Mtumba man,amekiri kwamba amekuwa  akipokea kichapo kutoka kwa mpenzi wake. 

Katika mahojiano ya moja kwa moja na Massawe Japanni kwenye Radio Jambo, Mtumba man alisema kwamba malumbano kati yake na mpenzi wake yamekuwa yakiendelea kwa muda mpaka pale alipoamua kuweka wazi kwa umma.

Alieleza kuwa si mazoea yake kumpiga mwanamke, na hivyo yeye hufanya kila awezalo wakati wa vita kujizuia ili asimuumize.

"Sijawahi kupiga mwanamke, na kila mara akianza vita, huwa namshika tu ili kuzuia vita kuendelea kwani sikuwahi taka kumuumiza."

Alisema zaidi kwamba, wamekuwa kwenye mahusiano kwa mwaka mmoja sasa na katika kipindi hicho amepokea kichapo cha maneno na vitendo kutoka kwa mpenzi wake.

Alieleza kuwa chanzo cha vita yao ni pale alipogundua kuwa mchumba wake anajihusisha na vitendo vya usagaji. Kulingana na yeye aligundua hili alipoichukua simu yake na kuchunguza alichokuwa anakishuku.

"Nilichukua simu yake, kuiangalia, nikapata video wakifanya vitendo vya ndoa na mwanamke fulani huku wakivuta sigara na kupigana mabusu,sikuamini nilichokiona, na hapo ndipo nilipomuuliza,lakini hakupenda nilichomuuliza na hapo akanisaba kofi." Alisema.

Mtumba Man anasema alivumilia tabia za mpenzi wake kwa sababu alikuwa ameamua kubadilisha maisha yake ili  kumsaidia kuepuka maudhui ya usagaji.

 Ameeleza kuwa kila mara baada ya malumbano, huwa wanasamehana na kurudi katika hali ya kawaida na kuendelea kwa sababu ya upendo alionao kwake.

Aidha amethibitisha kuwa, wakati mmoja aliwahi kumchoma na kisu wakati akimuuliza kuhusu vitendo vyake vya usagaji ambavyo anasema vinamkera.

Sande anasema, alijinyima mambo mengi sana ili kuhakikisha uhusiano wao unadumu mpaka pale itakapofikia wafunge ndoa ila kwa sasa hatma hiyo imemutoka.

Kero hizi zote amezivumilia akisema anajaribu kufanya kila awezalo kuendelea na msimamo wake  heshima kwa mwanamke. Akisema kuwa amepokea mawaidha mengi kutoka kwa marafiki kumpiga ila amekatalia msimamo wake.

"Si kwa sababu siwezi kumpiga,ila kwa sababu nina jina la kukuza,maana nafanya kazi na watu wengi sana na sitaki kudhalilisha heshima hiyo."

Sasa amesema kuwa ukali umekuwa tabia yake na kila akimuuliza  kuhusumakosa yoyote yeye huishia kumtandika, suala ambalo anahisi amechoka nalo hivyo kufikia uamuzi wa kuachana naye.